Lugha Nyingine
Uzuri wa Majira: Dongzhi-Solistasi ya Majira ya Baridi
Habari zenu, mimi ni Sisi, mpenda kutalii! Jumapili wiki hii itakuwa Dongzhi, au kipindi cha solistasi cha majira ya baridi, kinachoashiria mchana mfupi zaidi na usiku mrefu zaidi wa mwaka katika Nusu ya Kaskazini ya Dunia. Ungana nami tunapoingia Xi'an, mji uliokuwa mji mkuu wa enzi 13 nchini China, ili kujionea maelfu ya miaka ya historia yake na pilika na hali motomoto ya maisha ya wenyeji.
Kwa watu wa kale, Dongzhi ilikuwa mwanzo wa kuhesabu Vipindi 24 vya majira katika Kalenda ya kilimo ya China, ikiashiria mwanzo wa mzunguko mpya. Kama msemo unavyosema, "Kipindi cha solistasi cha majira ya baridi ni muhimu kama Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China." Siku hii inabeba matarajio mazuri ya kujumuika tena kwa familia na kuaga mambo ya zamani wakati huohuo kukaribisha mapya.
Katika mji wa Xi'an, ladha ya Dongzhi hupatikana kwenye bakuli la Jiaozi(dumplings) lenye kutoa mvuke. Watu wa Kaskazini mwa China hupenda Jiaozi. Hadithi inasema kwamba kula chakula hicho chenye umbo la masikio huzuia masikio kupigwa ganzi na baridi wakati wote wa majira ya baridi - bakuli moja la Jiaozi linajumuisha hekima ya kuzuia baridi. Wakati huo huo, kusini mwa China, Dongzhi haikamiliki bila tangyuan (vitafunwa vya mchele wenye kunata), ikiashiria kujumuika tena na kuwa pamoja.
Pamoja na Dongzhi huja desturi ya Wachina ya Shujiu, au "kuhesabu tisa." Wazee wa kale waligawanya siku 81 zilizofuata Dongzhi katika vipindi tisa zenye siku tisa kila moja, wakitunga wimbo wa jadi kuhusu "Vipindi tisa za Siku Tisa za Majira ya Baridi" ambao ulionyesha mabadiliko kutoka baridi kali hadi hali joto ya majira ya mchipuko.
Dongzhi si tu ni kipindi muhimu cha majira cha China, bali pia ni wakati wa unaosherehekewa pia katika tamaduni mbalimbali duniani. Nchini Korea Kusini, desturi ya kunywa uji wa maharagwe mekundu inatokana na imani ya kale ya "kuepuka mambo mabaya na maafa." Nchini Uingereza, kwenye mnara wa Neolithic wa Stonehenge, watu wengi hukusanyika kila mwaka siku hii kushuhudia jua likichomoza kupitia kwenye mawe. Ingawa muaumbo yake hutofautiana, yote yanaonyesha shauku ya pamoja ya mwanga, joto na kuwa pamoja.
Theluji inafunika Grand Tang Mall, ambako usanifu wa kale na taa zilizowashwa katika mpangilio wa mfululizo huleta maandhari ya kuvutia. Hapa Dongzhi inabeba vyote mvuto wa kale wa Enzi ya Tang yenye ustawi na furaha ya kisasa ya vijana wanaotembea wakiwa wamevalia mavazi ya kijadi ya Hanfu. "Mbingu na dunia hubadilika siku baada ya siku. Kuanzia kipindi cha Dongzhi, majira ya mchipuko yatakuja bila kuchelewa."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



