Alipotea akiwa baharini, akapatikana Afrika: safari maarufu ya ndege kozi mwenye miguu myekundu kutoka China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2025

Ndege kozi mwenye miguu myekundu akiruka angani. (Picha/VCG)

Ndege kozi mwenye miguu myekundu akiruka angani. (Picha/VCG)

JINAN - Katika safari yake kutoka kisiwa cha pwani mashariki mwa China hadi Bara la Afrika, ndege kozi mwenye miguu myekundu tayari amesharuka umbali wa kilomita 13,200.

Simulizi yake ilianza miezi miwili mapema kwenye kisiwa kidogo cha Daheishan katika Ghuba ya Bohai, sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Changdao katika mji wa pwani wa mashariki mwa China wa Yantai. Ndege huyo kozi mdogo, mwenye madoa meusi aligunduliwa kunaswa kwenye wavu Oktoba 15.

"Gramu mia mbili -- mkubwa kuliko majike wengi," mfanyakazi wa uhifadhi Han Xuetao alizungumza kwa kunong'ona kwenye simu. "Muwekee kisambaza mawimbi?" "Muwekee sasa hivi!" alihimiza Yu, katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuangalia Ndege ya Qingdao (QBA), akiwa upande wa pili wa mstari. "Ndege ambaye umbo linaweza kubeba simulizi." Alisema.

Han alimshikilia ndege huyo kwa upole na akaweka lebo ya gramu 3 mgongoni mwake kama mkoba mdogo, kabla ya ndege huyo, mwenye No. 7276 kwenye kanzidata, kuruka kuelekea angani.

Han na Yu ni miongoni mwa idadi inayoongezeka ya wahifadhi Wachina. Ndege kozi mwenye miguu myekundu, walioorodheshwa kwenye orodha ya spishi zinazolindwa kitaifa katika Daraja la II nchini China, wanafahamika sana kama ndege wa kuhama hama wa masafa marefu, lakini bado hawana data sahihi ya ufuatiliaji wa njia yao ya kuhama hama.

Nukta kwenye skrini ilifuatilia safari ya ndege huyo No. 7276: aliruka kusini kuvuka milima na mito ya China, juu ya Vietnam na Laos, kupumzika kwa wiki moja kwenye mashamba ya Myanmar, kisha kuruka kilomita 2,800 katika kipindi cha siku tano -- Bangladesh, India na kwenye ukingo unaong'aa wa Bahari ya Arabia.

Novemba 29, ndege huyo aliruka kutoka pwani ya India na nukta ya kumfuatilia kwenye ramani ikapotea. Ishara za satalaiti haziwezi kumfikia ndege juu ya bahari wazi. Kwa siku 3 na saa 18, timu hiyo ilikuwa ikikodolea macho skrini tupu, ikitazama kila baada ya saa moja au mbili, ikimfikiria akiwa peke yake juu ya kilomita 4,500 za maji.

Yu alipopata ishara ya kisambaza mawimbi katika saa za mapema siku hiyo, ndege huyo kozi alikuwa tayari ametua na alikuwa akitafuta chakula kwa utulivu kwenye vilima vya kusini mwa Tanzania. Mwisho wa safari yake ni maeneo ya kupita majira ya baridi yanayojulikana nchini Afrika Kusini.

"Kila mdundo wa mabawa uliopigwa ni data muhimu," amesema Yu, "taarifa hii itatoa msingi imara wa kisayansi wa kufahamu njia za ndege kozi kurukia na kulinda makazi yake."

"Njia ya kuhama hama ya ndege kozi imejidhihirisha wazi kama simulizi ya kusisimua," amesema Xue Lin, Mkuu wa QBA. “Watu wanapofuatilia safari ya ndege mmoja, wanaanza kujali kila ndege,” ameongeza.

China inatetea ushirikiano wa bioanuwai duniani. Mwezi Mei mwaka 2024, ilizindua Mfuko wa Bioanuwai wa Kunming (KBF) ili kusaidia mataifa yanayoendelea kulinda urithi wao wa viumbe hai. Miradi tisa ya kwanza ya ukubwa mdogo, inayotekelezwa katika nchi 15 katika mabara sita, tayari imeanza kutekeleza.

Oktoba mwaka huu, KBF iliidhinisha miradi 22 mipya yenye thamani ya dola za Marekani zaidi ya milioni 27 ambayo itanufaisha nchi 34 duniani kote.

Safari hiyo ya kusisimua ya ndege huyo No. 7276 haijakamilika. Majira yajayo ya mchipuko nchini China, ataelekea kaskazini tena, akirudi kupita barabara yake ya kuvuka bahari. "Tutakuwa tukisubiri kisiwani," Yu amesema.

Mfanyakazi wa uhifadhi akiweka kisambaza mawimbi kwenye ndege kozi mwenye miguu myekundu katika kisiwa kidogo cha Daheishan, sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Changdao katika Mji wa Yantai, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Oktoba 15, 2025. (Xinhua)

Mfanyakazi wa uhifadhi akiweka kisambaza mawimbi kwenye ndege kozi mwenye miguu myekundu katika kisiwa kidogo cha Daheishan, sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Changdao katika Mji wa Yantai, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Oktoba 15, 2025. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha