Lugha Nyingine
China yaihimiza Marekani kuacha "kitendo hatari" kufuatia idhini ya Marekani ya mauzo makubwa ya silaha kwa Taiwan
BEIJING - Marekani inapaswa kuacha mara moja "kitendo chake cha hatari" cha kuiuzia Taiwan silaha, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun alisema jana Alhamisi alipotoa maelezo kuhusu idhini ya Marekani juu ya mpango wake wa mauzo ya silaha chenye thamani ya dola za Marekani takriban bilioni 11 kwa eneo la Taiwan.
"Marekani ilitangaza waziwazi mpango wake wa kuuza silaha nyingi za hali ya juu kwa eneo la Taiwan la China, jambo ambalo linakiuka vibaya kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani," Guo amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Amesema hatua hiyo ya Marekani inakiuka mamlaka ya nchi, usalama na ukamilifu wa ardhi ya China, inaharibu amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan, na inatoa ishara ya makosa kabisa kwa nguvu ya mafarakano ya kutaka "Taiwan Ijitenge".
"China inapinga kithabiti na inalaani vikali," amesema.
Amesema, nguvu ya mafarakano ya kisiwani humo ya kutaka "Taiwan Ijitenge" inajaribu kusukuma mbele ajenda yake ya "kujitenga" na kukataa muungano kwa kupitia upanuzi wake wa kijeshi, kufuja pesa za walipa kodi kwa kununua silaha, na hata kunawezekana kubadilisha Taiwan kuwa "kapu la baruti".
Guo amesema hatua kama hizo hazitaweza kubadilisha ukweli wa mambo wa kushindwa kusikoepukika kwa "Taiwan Kujitenga," na zitasukuma tu kwa haraka Mlango-Bahari wa Taiwan katika hatari ya migogoro ya kijeshi. "Kwa Marekani, kusaidia ajenda ya "kujitenga" kwa kuizatiti Taiwan silaha kutaleta matokeo mabaya tu kwake, na kuitumia Taiwan kuizuia China hakutafanikiwa kamwe, " ameongeza.
Msemaji huyo amesisitiza kuwa suala la Taiwan liko katika kiini cha maslahi ya msingi ya China, na ni mstari wa kwanza mwekundu ambao haupaswi kuvukwa katika uhusiano kati ya China na Marekani, Guo amesema hakuna mtu atakayeweza kupuuza nia thabiti na uwezo mkubwa wa serikali ya China na watu wa China katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China.
"China inaihimiza Marekani kutii kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, kutekeleza ahadi nzito za viongozi wake, na kuacha mara moja kitendo cha hatari cha kuipa Taiwan silaha, " amesema.
Msemaji huyo ameongeza kusema kuwa, China itachukua hatua thabiti yenye nguvu kwa kulinda mamlaka ya nchi, usalama na ukamilifu wa ardhi ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



