Mjumbe maalum wa China kuzipatanisha Cambodia na Thailand

(CRI Online) Desemba 18, 2025

Mjumbe Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China anayeshughulikia masuala ya Asia, leo Alhamisi atafanya tena safari ya kuhimiza diplomasia kati ya Cambodia na Thailand ikiwa ni sehemu ya juhudi ya kuzileta pamoja pande hizo mbili ili kujenga upya amani katika siku za mapema.

Msemaji wa Wizara hiyo amesema ikiwa ni jirani na rafiki wa karibu wa Cambodia na Thailand, China inafuatilia kwa karibu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya nchi hizo mbili, na kwamba imekuwa ikifanya safari za kuhimiza diplomasia kati ya pande hizo mbili ili kuhimiza amani.

"Kupitia njia yake yenyewe, China imekuwa ikifanya kazi kwa juhudi zote kutuliza hali," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha