Somalia yaadhimisha miaka 65 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China

(CRI Online) Desemba 18, 2025

Somalia na China zimesherehekea miaka 65 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia huku zikiahidi kuinua ushirikiano na kufuata maslahi zaidi ya pamoja.

"Tunakusanyika kusherehea hatua muhimu ya kweli ya kihistoria, miaka 65 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Somalia na China. Haya ni maadhimisho muhimu, ushuhuda wa urafiki wa kudumu kati ya watu wetu, urafiki uliojengwa kwa kuheshimiana, mamlaka, na maelewano" Waziri Mkuu wa Somalia Bw. Hamza Abdi Barre amesema kwenye hafla iliyofanyika mjini Mogadishu jana Jumatano.

Bw. Abdi amesema tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1960, Somalia na China zimekuwa pamoja kupita nyakati zinazobadilika, maendeleo na changamoto, na mabadiliko ya kikanda na kimataifa.

Pia amesema kwa miongo kadhaa sasa, China imeendelea kuwa mshirika anayeaminika, anayeheshimu uhuru, na anayeunga mkono vipaumbele vya kitaifa vya Somalia.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha