Lugha Nyingine
Timu ya 17 ya Madaktari wa China yawasili Comoro ili kuimarisha ushirikiano wa mambo ya afya

Balozi wa China nchini Comoro Huang Zheng (wa kwanza kushoto) na Waziri wa Afya na Ulinzi wa Jamii wa Comoro Ahamadi Sidi Nahouda (wa pili kulia) kwa pamoja wakimkabidhi cheti cha heshima mjumbe wa timu ya 16 ya madaktari wa China nchini Comoro kwenye hafla ya kusherehekea kuwasili kwa Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro na kuondoka kwa timu ya 16 huko Moroni, mji mkuu wa Comoro, Desemba 15, 2025. (Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro/kupitia Xinhua)
ANTANANARIVO – Hafla ya kusherehekea kuwasili kwa Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro na kuondoka kwa timu ya 16 imefanyika Jumatatu huko Moroni, mji mkuu wa Comoro, ikionyesha ushirikiano unaoendelea wa pande mbili katika mambo ya afya.
Kwenye hafla hiyo, Waziri wa Afya na Ulinzi wa Jamii wa Comoro Ahamadi Sidi Nahouda alizisifu timu za madaktari za China kwa huduma zao.
"Kupitia kujitolea kwenu kila siku, mmetoa mchango muhimu katika kuimarisha mfumo wetu wa afya na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya," waziri huyo amesema.
Amesema kwamba timu za madaktari wa China, zikiwa ni "mashuhuda waliobahatika" kwa hali halisi ya kila siku ya Comoro, zitaendelea kuwa "mabalozi wa urafiki kati ya China na Comoro," zikibeba matarajio makubwa ya watu wa Comoro kwa afya, upigaji hatua na amani.
Balozi wa China nchini Comoro Huang Zheng amesema kutumwa kwa timu za 16 na 17 za madaktari wa China kwenda Comoro kumeonesha kazi ya vielelezo ya mpango wa utendaji wa ushirikiano wa mambo ya afya uliotolewa kwenye Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika la mwaka 2024.
Balozi huyo amesema kwamba timu ya 16 ya madaktari wa China imekamilisha jukumu lake kwa mafanikio, na ameelezea matumaini yake kwamba timu ya 17 ya madaktari wa China itaendelea kusukuma mbele urafiki kati ya China na Comoro kwa kupitia huduma zao za matibabu za kitaaluma, kufuata maadili ya matibabu na kutoa mchango bila kulegalega.
Su Yunyu, mkuu wa timu ya 17 ya madaktari wa China nchini Comoro, amesema timu hiyo mpya ina wataalamu 11 waliobobea katika upasuaji wa jumla, mifupa, uzazi na magonjwa ya wanawake, na matibabu ya jadi ya China.
Tangu mwaka 1994, China imekuwa ikituma timu za madaktari wa China kwenda Comoro, nchi ya visiwa ya magharibi mwa Bahari ya Hindi, zikitoa huduma za matibabu kwa wagonjwa kwa zaidi ya mara 600,000 hadi kufikia Novemba mwaka huu.

Waziri wa Afya na Ulinzi wa Jamii wa Comoro Ahamadi Sidi Nahouda akizungumza kwenye hafla ya kusherehekea kuwasili kwa Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro na kuondoka kwa timu ya 16 mjini Moroni, mji mkuu wa Comoro, Desemba 15, 2025. (Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro/kupitia Xinhua)

Su Yunyu mkuu wa Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro akizungumza kwenye hafla ya kusherehekea kuwasili kwa Timu ya 17 ya Madaktari na kuondoka kwa timu ya 17 mjini Moroni, mji mkuu wa Comoro, Desemba 15, 2025. (Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro/kupitia Xinhua)

Balozi wa China nchini Comoro Huang Zheng akizungumza kwenye hafla ya kusherehekea kuwasili kwa Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro na kuondoka kwa timu ya 16 mjini Moroni, mji mkuu wa Comoro, Desemba 15, 2025. (Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro/kupitia Xinhua)

Balozi wa China nchini Comoro Huang Zheng (wa kwanza kushoto) na Waziri wa Afya na Ulinzi wa Jamii wa Comoro Ahamadi Sidi Nahouda (wa pili kulia) kwa pamoja wakimkabidhi cheti cha heshima mjumbe wa timu ya 16 ya madaktari wa China nchini Comoro, Desemba 15, 2025. (Timu ya 17 ya Madaktari wa China nchini Comoro/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



