Hainan 101: Bandari ya Biashara Huria na Uendeshaji Maalum wa Forodha vyafafanuliwa | Je, ni kitu gani hasa?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2025

Kuanzia Desemba 18, 2025, Bandari ya Biashara Huria ya Hainan itazindua rasmi uendeshaji maalumu wa forodha kisiwani kote, ambao utafanya mkoa huo wa Hainan wa China kuwa eneo lililofungua mlango la forodha maalumu.

Lakini hiyo inamaanisha nini hasa? Ni mambo gani yanahusu uendeshaji maalumu wa forodha, na ni kwa namna gani yatabadilisha maisha na biashara ya kila siku mkoani Hainan? Ili kupata majibu dhahiri, Michael Kurtagh kutoka People's Daily Online alifunga safari kwa ajili ya kwenda kujionea mwenyewe uhalisia wa mambo katika sehemu mbalimbali kisiwani Hainan.

Kwenye Bandari ya Kimataifa ya Makontena ya Yangpu, alitazama jinsi bidhaa zinavyohamishwa kwa kasi mpya. Kwenye Maduka ya Kimataifa yasiyotoza Ushuru ya Sanya, alijaribu ofa mpya zaidi kwa wateja. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Meilan, aliona jinsi safari zinavyozidi kurahisishwa. Na kwenye Jumuiya ya Vipaji vya Kimataifa ya Haikou, alifahamishwa namna Hainan inavyovutia wataalamu kutoka nchi zote duniani.

Baada ya siku kadhaa za mahojiano ya hapo papo, mandhari za kujionea moja kwa moja ana kwa ana, na waelezeaji wa sera kwa urahisi, moyo wa uendeshaji huo maalumu wa forodha umekuwa dhahiri. Kila kitu kinakuja kwenye hitimisho la mambo matatu makuu ambayo kila mmoja anaweza kuyaelewa: mtirirko huria zaidi, uokoaji mkubwa zaidi wa pesa, na fursa mpya.

Je, upo tayari kuzama kwenye zama mpya ya Hainan ya uhuria na uwezekano? Ungana nasi kwa kipindi cha kwanza cha safari hii ya vipindi vitatu!

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha