China yakataa kithabiti jibu lisilo na nia ya dhati la Waziri Mkuu wa Japan la "hakuna mabadiliko katika msimamo kuhusu Taiwan"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2025

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesema China inakataa jibu lisilo na nia ya dhati la Waziri Mkuu wa Japan la "hakuna mabadiliko katika msimamo kuhusu Taiwan", na inauhimiza upande wa Japan urudishe maneno ya makosa aliyoyasema waziri mkuu wake kuhusu Taiwan.

Lin amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Alhamisi mjini Beijing wakati akijibu swali linalohusu baadhi ya habari zilizotolewa na vyombo vya habari, ambazo zilisema kuwa kwenye mkutano wa wajumbe wote wa baraza la juu Desemba 3, Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi alirejelea Taarifa ya Pamoja kati ya China na Japan, akisema kwamba upande wa Japan "unaelewa na kuheshimu" msimamo wa serikali ya China kwamba "Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya ardhi ya Jamhuri ya Watu wa China."

Lin amesema habari hizo zimethibitishwa kuwa si ya sahihi, amesema kuwa Waziri Mkuu wa Japan alisema tu "msimamo wa kimsingi wa serikali ya Japan kuhusu Taiwan unabaki kama ilivyoelezwa kwenye Taarifa ya Pamoja kati ya China na Japan ya 1972, msimamo huo haujabadilika, na hakusema mengine zaidi."

"Msimamo wa China uko wazi sana: Tunauhimiza upande wa Japan kujikosoa na kurekebisha makosa yake, na kurudisha maneno ya makosa ya Waziri Mkuu Takaichi. Hili ni suala la kikanuni," amesisitiza.

"China imekuwa ikiuuliza upande wa Japan maswali yaleyale kwa siku nyingi na bado haijapata jibu, na wengi pia wamekosoa maneno aliyosema Waziri Mkuu Takaichi ndani na nje ya Japan, sasa alisema tu msimamo haujabadilika, hayo hayajatosha kabisa na hakika hayawezekani kuchukuliwa kuwa ni jibu lake kwa China," Lin amesema, akieleza kuwa ukweli wa mambo na ahadi za Japan vyote vimewekwa kuwa kumbukumbu kwenye rekodi za kihistoria.

"Kama msimamo wa kimsingi wa upande wa Japan kuhusu Taiwan ni kweli kama ilivyoelezwa kwenye Taarifa ya Pamoja kati ya China na Japan ya 1972, je, Waziri Mkuu Takaichi anaweza kuelezea msimamo huo kwa usahihi na kikamilifu au la? Kwa nini upande wa Japan haupendi kueleza waziwazi ahadi ulizotoa na wajibu wake wa kisheria? Ni mantiki na nia gani zinazochochea msimamo wake huu?" Lin ameuliza.

"Upande wa Japan unapaswa kutoa maelezo yake kwa China na jumuiya ya kimataifa" msemaji ameongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha