Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kuacha mawasiliano yake ya kiserikali na Taiwan
BEIJING – Msemaji wa Wizaa ya mambo ya nje ya China jana Jumatano amesema kuwa, China inapinga kwa uthabiti aina yoyote ya mawasiliano ya kiserikali ya upande wa Marekani na eneo la Taiwan la China, na inaihimiza Marekani kuacha mawasiliano yake ya kiserikali na Taiwan na kuepusha kutoa ishara yoyote ya makosa kwa nguvu ya mafarakano ya kuitaka "Taiwan Ijitenge".
Habari zimesema kwamba Rais wa Marekani Donald Trump amesaini kwenye sheria ambayo inaitaka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kupitia mara kwa mara hali ya mawasiliano kati ya Marekani na Taiwan, na kutafuta njia za kuzidisha mawasiliano na Taiwan.
Kwa hali hiyo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian jana Jumatano alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing kwamba China inapinga kwa uthabiti aina yoyote ya mawasiliano ya kiserikali ya upande wa Marekani na eneo la Taiwan la China, na msimamo huo ni wa siku zote na waziwazi bila kubadilika.
Amesema, suala la Taiwan linahusiana na kiini cha maslahi ya China, na ni mstari wa kwanza mwekundu ambao hauwezi kuvukwa katika uhusiano kati ya China na Marekani.
Amesema kanuni ya kuwepo kwa China moja ndiyo msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani, na serikali ya Marekani ilitoa ahadi wazi katika taarifa ya pamoja juu ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kwamba “Marekani inatambua Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa ni serikali pekee halali ya China. Katika muktadha huu, watu wa Marekani watadumisha mawasiliano ya kiutamaduni na kibiashara na watu wa Taiwan, na mawasiliano mengine yasiyo ya kiserikali."
"China inauhimiza upande wa Marekani kufuata kwa makini kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, kuchukua tahadhari zaidi wakati wa kushughulikia suala la Taiwan, kuacha mawasiliano yake ya kiserikali na Taiwan, na kuacha kutoa ishara yoyote ya makosa kwa nguvu ya mafarakano ya kuitaka "Taiwan Ijitenge," Lin amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



