China na Russia kuendeleza uratibu wa kimkakati kuwa na sifa bora zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2025

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Russia, wakiongoza kwa pamoja duru ya 20 ya mashauriano ya usalama wa kimkakati kati ya China na Russia mjini Moscow, Russia, Desemba 2, 2025. (Xinhua/Hao Jianwei)

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Russia, wakiongoza kwa pamoja duru ya 20 ya mashauriano ya usalama wa kimkakati kati ya China na Russia mjini Moscow, Russia, Desemba 2, 2025. (Xinhua/Hao Jianwei)

MOSCOW - China na Russia zimekubaliana kutekeleza kikamilifu makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili juu ya usalama wa kimkakati na kusukuma mbele uratibu wa kimkakati wa pande mbili kuwa wa sifa bora zaidi.

Makubaliano hayo yamefikiwa jana Jumanne kwenye mkutano kati ya Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya kamati kuu ya CPC, na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Russia.

Wang na Shoigu waliongoza kwa pamoja duru ya 20 ya mashauriano ya usalama wa kimkakati kati ya China na Russia, ambapo pande hizo mbili zimefanya mazungumzo ya pande zote na ya kina juu ya masuala makubwa yanayohusu maslahi ya kimkakati ya usalama wa nchi zote mbili, kufikia makubaliano mapya, na kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati.

Wang amesema kuwa uhusiano kati ya China na Russia umepata maendeleo ya kiwango cha juu zaidi mwaka huu. Amesema, hasa Rais Xi Jinping wa China na Rais Vladimir Putin wa Russia walikutana mara mbili mwaka huu, mara moja mjini Moscow na mara nyingine mjini Beijing, wakitoa mwongozo kwa kuhimiza maendeleo tulivu ya uhusiano wa pande mbili chini ya mazingira magumu na yanayobadilika.

"Mwaka ujao ni maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa uratibu wa kimkakati kati ya China na Russia na maadhimisho ya miaka 25 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema na Ushirikiano wa Kirafiki kati ya China na Russia, na ni hatua muhimu katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia katika zama mpya," Wang amebainisha.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati, kuzidisha ujirani mwema na urafiki mzuri, na kupanua ushirikiano wa kunufaishana ili kuhudumia maendeleo ya uchumi na ustawishaji wa kitaifa ya kila upande, kukabiliana kwa pamoja na matishio na changamoto zinazoibuka, na kulinda vyema haki, usawa, amani na utulivu duniani.

Wang amesema kuwa mfumo wa mashauriano ya usalama wa kimkakati kati ya China na Russia ni njia muhimu kwa nchi hizo mbili kuzungumza kwa kina juu ya masuala makubwa kuhusu usalama wa kimataifa na utulivu wa kimkakati, na pia ni jukwaa muhimu ya uratibu wa kimkakatikwa ajili ya kulinda maslahi ya msingi ya pande zote mbili.

Wang amezihimiza pande zote mbili kuendelea kutumia kikamilifu mfumo huo, kuimarisha mawasiliano na uratibu wa kimkakati, na kukabiliana kwa pamoja changamoto za nje.

Kwa upande wake Shoigu amesema Russia na China zinahitaji kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kwani mazingira ya siasa za kijiografia ya kimataifa yanapitia mabadiliko magumu na changamoto za usalama duniani zinaongezeka.

"Uratibu wa kimkakati kati ya Russia na China uko katika kiwango cha juu ambayo haijawahi kutokea, ambayo inaendana na maslahi ya kitaifa ya nchi zote mbili na inanufaisha amani ya kikanda na kimataifa," Shoigu amesema.

Amesema kuwa Russia inashikilia kithabi kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaunga mkono kithabiti misimamo ya China juu ya Taiwan, Xizang, Xinjiang na Hong Kong. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha