Lugha Nyingine
China yasema Japan kuweka silaha za mashambulizi karibu na Taiwan ya China kunahitaji jumuiya ya kimataifa kukaa macho zaidi
BEIJING - Akijibu swali jana Jumatatu kuhusu mpango wa Japan wa kuweka silaha za mashambulizi karibu na eneo la Taiwan la China, Mao Ning, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema hatua hiyo ni hatari sana, akitoa wito wa kutaka nchi jirani na jumuiya ya kimataifa kukaa macho zaidi.
Msemaji Mao amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, akisema kuwa vitendo hivyo vya Japan vinaongeza kwa makusudi hali wasiwasi ya kikanda na kuchochea mapambano ya kijeshi.
"Kwa kuzingatia kauli potofu ya Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi kuhusu Taiwan, hii ni hatua yenye hatari kubwa kabisa na inahitaji nchi jirani na jumuiya ya kimataifa kudumisha hali ya kukaa kwa macho zaidi," ameongeza.
Msemaji Mao amesema Tangazo la Potsdam limeamua bayana kwamba Japan hairuhusiwi "kujizatiti upya kwa silaha kwa ajili ya vita," akiongeza kuwa Katiba ya Nchi ya Japan, ambayo inasisitiza amani, pia imeweka sera ya Japan ya kujikita katika ulinzi wake.
"Lakini hali inayowataka watu kukaa kwa macho zaidi ni kwamba, katika miaka ya hivi karibuni, Japan imerekebisha kwa kiasi kikubwa sera yake ya usalama na ulinzi, imekuwa ikiongeza bajeti ya ulinzi mwaka baada ya mwaka, imepunguza ukomo wa kuuza silaha nje ya nchi, imejaribu kutafuta kutengeneza silaha za mashambulizi, na imepanga kuacha utekelezaji wa kanuni zake tatu za kutokuwa na nyuklia," msemaji Mao ameongeza.
"Wachochezi wa mrengo wa kulia wa Japan wanajaribu kutumia kila namna kujitoa kwenye vizuizi vya katiba ya nchi ya amani, wakifuata zaidi upanuzi wa silaha na kuifanya Japan na kanda nzima kuelekea matokeo ya balaa," msemaji huyo amesema.
Huku akibainisha mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Taiwan kujitoa kwenye utawala wa Japan, China haitaruhusu kamwe nguvu ya mrengo mkali wa kulia nchini Japan kurudisha nyuma mwelekeo wa historia, wala kuruhusu uingiliaji kati wowote wa nje ya mambo ya eneo la Taiwan, au kuiruhusu Japan kufufua tena matumizi ya nguvu za kijeshi ya Japan.
Msemaji huyo pia amesema kuwa China ina dhamiria na uwezo wa kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



