Lugha Nyingine
Mpango wa muunganisho wa miundombinu kati ya China na Singapore wapata matokeo makubwa

Picha hii iliyopigwa Septemba 30, 2021 ikionyesha eneo la biashara la Jiefangbei (juu) na eneo la kivutio cha watalii la Shibati mjini Chongqing, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Huang Wei)
CHONGQING - Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Mpango wa Kielelezo kati ya China na Singapore (Chongqing) kuhusu Muunganisho wa Kimkakati wa Miundombinu umeibuka kuwa mradi kinara kwa ushirikiano wa kimataifa, ukiimarisha kwa mafanikio muunganisho wa miundombinu kati ya maeneo ya magharibi mwa China na Asia ya Kusini Mashariki.
Ukiadhimisha miaka yake 10 tangu kuanzishwa, mpango huo, uliozinduliwa Novemba 7, 2015, unasimama kama ushirikiano mkubwa wa tatu wa kati ya serikali kati ya China na Singapore, kufuatia Eneo Maalum la Viwanda la Suzhou la China na Singapore mashariki mwa China na Mji wa Ikolojia wa Tianjin wa China na Singapore kaskazini mwa China.
Mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu wiki hii ulisisitiza mafanikio matano muhimu yanayohusiana na biashara, ufadhili, takwimu, muunganisho wa anga na mawasiliano kati ya watu, yote yakizingatiwa kama hatua muhimu za kuimarisha ushirikiano wa muunganisho.
Mkutano huo umerejelea Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa wa Nchi Kavu na Baharini, ambao umekuwa ni njia ya usafirishaji kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).
Ilisemwa kwenye mkutano huo na waandishi wa habari kwamba, hadi kufika mwishoni mwa Oktoba, ushoroba huo ulikuwa umeunganisha kwenye bandari 581 katika nchi na maeneo 127, ukisaidia kuongeza thamani ya biashara kati ya maeneo ya magharibi mwa China na ASEAN hadi kufikia yuan zaidi ya trilioni 1 (dola za Kimarekani karibu bilioni 141) -- ongezeko kubwa la asilimia 75.3 tangu kuzinduliwa kwake.
Imeripotiwa kwenye mkutano huo kwamba, katika kurahisisha mtiririko wa mitaji kwa ajili ya BRI, ushoroba wa ufadhili wa kuvuka mipaka umeongeza thamani ya jumla ya ufadhili wa kuvuka mipaka wa dola bilioni 21.7 za Marekani katika muongo huo mmoja uliopita.
Imeelezwa kuwa, mawasiliano kati ya watu pia kumeongezeka pamoja na biashara ya pande mbili.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa njia ya ndege kati ya Chongqing na Singapore ilishuhudia safari 252,400 za abiria mwaka 2024 -- ongezeko la asilimia 237.3 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kwa mujibu Sun Xiyong, naibu mkurugenzi wa Kamisheni ya Biashara ya Chongqing ambaye pia ameongeza kuwa pande hizo mbili pia zimekuwa maeneo makuu vya utalii kwa watu wa upande mwingine, huku shughuli za kitamaduni yenye maudhui maalumu yakigeuka kuwa majukwaa muhimu ya mawasiliano ya kitamaduni.
"Tofauti na miradi ya Suzhou na Tianjin, Mpango wa Kielelezo kati ya China na Singapore wa Chongqing unatambuliwa kipekee kwa kuimarisha muunganisho, kuchochea maendeleo magharibi mwa China na kuanzisha uvumbuzi wa kitaasisi," amesema Li An, naibu mkuu wa idara ya masuala ya Asia ya Wizara ya Biashara ya China.
"Huu siyo tu mradi kinara wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa China na Singapore -- lakini pia umekuwa jukwaa muhimu kwa maeneo ya ndani ya magharibi mwa China kwenda kimataifa." ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



