Naibu Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kuimarisha ushirikiano na Norway

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2025

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa  Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing, China,  Novemba 11, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing, China, Novemba 11, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING – Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kivitendo katika sekta mbalimbali alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing jana Jumanne.

Ding, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kwamba watu wa China na Norway wanafurahia urafiki wa jadi, na uhusiano wa pande mbili umedumisha maendeleo mazuri na tulivu.

"Viongozi wa nchi mbili walifikia maoni muhimu ya pamoja juu ya kusukuma mbele uhusiano wakati wa mkutano wao mwaka jana" ameongeza.

Aidha, ameeleza kuwa mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC, ambao ulielezea mpango wa maendeleo ya China katika kipindi cha miaka mitano ijayo, utatoa fursa zaidi kwa ushirikiano kati ya China na Norway.

Amehimiza kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, na kuongeza ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara, uwekezaji, mabadiliko ya muundo wa kijani na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Waziri Eide amesifu sana mafanikio dhahiri yalipatikana nchini China katika mabadiliko ya muundo wa kijani na maeneo mengine, akisema Norway inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na ina matumaini ya kuboresha uhusiano wa pande mbili na kuufanya ushirikiano uendelee kwenye kiwango kipya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha