Lugha Nyingine
China yalitaka Bunge la Ulaya lisitume ishara mbaya kwa nguvu inayotaka "Taiwan Ijitenge"
BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema kwamba China imeeleza kupinga Bunge la Ulaya kuwaacha wanasiasa wa kutaka "Taiwan Ijitenge" kuhudhuria kwenye "mkutano wa Muungano wa Mabunge" ndani ya jengo la Bunge la Ulaya.
Lin alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatatu alipoulizwa kuhusu kuimarishwa kwa "ufikiaji" na Taiwan kwa Ulaya, wakati Tsai Ing-wen akitarajia kutoa hotuba mjini Berlin siku hiyo hiyo. Kabla ya hayo, Hsiao Bi-khim wa Taiwan alitoa hotuba ya ajabu katika kundi moja la Bunge la Ulaya mjini Brussels Ijumaa wiki iliyopita, akitoa wito wa kutaka kupata uungaji mkono zaidi kwa Taiwan.
Msemaji huyo amesema, "Upande wa Ulaya umesema kuwa ahadi ya Bunge la Ulaya kwa sera ya kuwepo kwa China moja haijabadilika na pia haitabadilika. Mkutano husika haukufanyika kutokana na mwaliko wa Bunge la Ulaya, watu husika hawakualikwa na bunge hilo na viongozi wa bunge hilo hawakuwa na mawasiliano yoyote nao. Vitendo binafsi vya Wabunge binafsi wa Bunge la Ulaya (MEPs) haviwakilishi msimamo rasmi wa Bunge la Ulaya."
Akibainisha kwamba Muungano wa Mabunge (IPAC) unafadhiliwa na mashirika kadha wa kadha yanayopinga China na umezoea kueneza habari potofu kuhusu China, Lin amesema, utawala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (DPP) unatumia IPAC, kundi ambalo halina uaminifu wowote, kuomba uungaji mkono wa kigeni kwa ajenda yake ya kujitenga.
"Maigizo ya kisiasa yanayofanywa na wanasiasa wa kutaka 'Taiwan Ijitenge' na IPAC yanalenga tu kuvutia ufuatiliaji wa watu. Majaribio kama hayo hayatafanikiwa," Lin amesema.
Amesisitiza tena kwamba haijalishi utawala wa DPP na nguvu ya mafarakano ya kutaka "Taiwan Ijitenge" vinajaribu kugeukia nini na kuongeza "ufikiaji" wao wowote, utafanya tu njama yao ya kujitenga ionekane wazi zaidi na kamwe hautaweza kuzuia muungano wa China.
"Tunatumai Bunge la Ulaya halitaelewa kwa makosa kuhusu hali halisi ya utawala wa DPP, kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, kutotoa ishara yoyote ya makosa kwa nguvu ya kutaka 'Taiwan Ijitenge', na kuepuka kujitumiwa," amesema.
Msemaji huyo pia ameihimiza Ujerumani kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, kupinga waziwazi vitendo vyote vya kuitaka "Taiwan Ijitenge", kutotoa ishara yoyote ya makosa kwa nguvu ya mafarakano ya kutaka "Taiwan Ijitenge", na kudumisha kihalisi hali nzima ya uhusiano kati ya pande mbili za China na Ujerumani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



