ICRC: Mgogoro wa kutumia silaha wasababisha watu zaidi ya 445,000 nchini Sudan Kusini kukimbia makazi

(CRI Online) Novemba 05, 2025

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema katika taarifan yake jana Jumanne kuwa, watu zaidi 445,000 nchini Sudan Kusini wamelazimika kukimbia makazi yao mwaka 2025 kutokana na kuongezeka kwa mapigano nchini humo, ikizidisha moja ya misukosuko ya muda mrefu zaidi ya kibinadamu duniani.

Kamati hiyo imesema athari za pamoja za mgogoro wa Sudan Kusini na Sudan, vurugu za mara kwa mara kati ya makabila, na mafuriko makubwa vimekuwa na athari mbaya kwa jamii katika mwaka huu.

ICRC imesema, familia nyingi zinakabiliwa na hali ngumu na sintofahamu kutokana na ufadhili wa misaada kupungua kwa kiasi kikubwa huku huduma muhimu zikikabiliwa na ukosefu wa fedha.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha