AU yatoa wito wa hatua zenye ufanisi ili kulinda mazingira ya asili kwa ustawi wa bara hilo

(CRI Online) Novemba 05, 2025

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulika na Kilimo, Maendeleo Vijijini, Uchumi wa Bluu na Mazingira Endelevu Moses Vilakati akizungumza katika Kikao cha kwanza cha Mawaziri cha Mkutano wa Bioanuwai wa Afrika mjini Gaborone, Botswana, Novemba 4, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Umoja wa Afrika umetoa wito kwa nchi wanachama wake kuchukua hatua za kiufanisi ili kulinda mazingira ya asili kwa ustawi na uhai wa bara hilo.

Akizungumza jana Jumanne kwenye kikao cha kwanza cha ngazi ya Mawaziri cha Mkutano wa Bioanuwai wa Afrika, uliofanyika katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulika na Kilimo, Maendeleo ya Vijijini, Uchumi wa Bluu na Mazingira Endelevu Moses Vilakati, ametoa wito kwa juhudi za kuimarisha sera na uwekezaji katika mazingira ya asili.

Amesema Bioanuwai si suala lisilo la muhimu bali ni msingi wa uchumi, mifumo ya chakula, afya, na utambulisho wa kiutamaduni. Amesisitiza haja ya mifumo imara ya sera, uwekezaji katika suluhu ambazo msingi wake ni mazingira ya asili, na kuwezesha vijana na jamii za wenyeji kuwa viongozi wa uhifadhi ili kutimiza Ajenda ya AU ya mwaka 2063 kwa ajili ya Afrika yenye mafungamano na ustawi.

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulika na Kilimo, Maendeleo Vijijini, Uchumi wa Bluu na Mazingira Endelevu Moses Vilakati (kwenye mimbari) akizungumza katika Kikao cha kwanza cha Mawaziri cha Mkutano wa Bioanuwai wa Afrika mjini Gaborone, Botswana, Novemba 4, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha