Afrika Kusini yatoa ripoti ya G20 ikionya kuhusu msukosuko wa hali isiyo na usawa duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2025

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kushoto) akipokea Ripoti ya Kamati Maalum ya G20 juu ya Hali isiyo na Usawa Duniani kutoka kwa Mshindi wa Tuzo ya Nobel Joseph Stiglitz kwenye hafla iliyofanyika Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 4, 2025. (Picha na Shakirah Thebus/Xinhua)

CAPE TOWN - Ripoti ya Kamati Maalum ya G20 juu ya Hali isiyo na Usawa Duniani iliyotolewa wakati Afrika Kusini ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa kamati hiyo imetoa onyo juu ya msukosuko unaozidi kuwa mbaya wa hali isiyo na usawa duniani, ikitoa wito wa kuundwa kwa kamati mpya ya kimataifa ili kutoa uelekezaji kwa utungaji sera wa nchi mbalimbali duniani.

Jana Jumanne, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alipokea Ripoti hiyo kutoka kwa Mshindi wa Tuzo ya Nobel Joseph Stiglitz, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima, na wataalamu wengine wanne wakuu wa kimataifa wa kamati hiyo kwenye hafla iliyofanyika Cape Town.

Ripoti hiyo, iliyoratibiwa na Kamati Maalum ya Kujiamulia ya Wataalamu juu ya Hali isiyo na Usawa Duniani, iliagizwa na Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini akiwa mwenyekiti wa zamu wa G20 chini ya kaulimbiu ya "Mshikamano, Usawa, Uendelevu". Imeonya kwamba kati ya mwaka 2000 na 2024, watu wenye utajiri zaidi wanaochukua asilimia moja duniani wamechukua asilimia 41 ya mali zote zilizoongezwa.

Kulingana na ripoti hiyo, asilimia 83 ya nchi zenye asilimia 90 ya idadi ya watu wote duniani, sasa zinalingana na ufafanuzi wa Benki ya Dunia wa "hali isiyo na usawa" ambapo nchi hizo zina uwezekano wa mara saba zaidi wa kutokea hali ya kudidimia kidemokrasia kuliko jamii zenye hali ya usawa zaidi.

Takwimu zilizotolewa na Maabara ya Hali isiyo na Usawa Duniani zimeonesha kuwa, asilimia moja ya watu tajiri zaidi duniani kwa wastani wao wameongeza mali kwa dola milioni 1.3 za Marekani tangu mwaka 2000, wakati huohuo asilimia 50 ya watu maskini zaidi wamepata dola 585 za Marekani kwa wastani (zilizorekebishwa kwa mfumuko wa bei).

Ripoti hiyo inasema, ingawa pengo la mapato kati ya watu binafsi limepungua kwa sababu za ukuaji nchini China, lakini tofauti kubwa ya utajiri kati ya nchi za Kaskazini na nchi za Kusini mwa Dunia imeonekana kuwa ya wazi sana.

"Dunia inaelewa kwamba tunakabiliwa na hali ya dharura ya tabianchi; ni wakati wa kutambua kwamba tunakabiliwa na msukosuko wa hali isiyo na usawa pia," amesema Stiglitz, ambaye alikuwa mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ya watu sita walioandaa ripoti hiyo.

Amesema, utajiri mwingi ulio wa juu unatokana na "mamlaka ya ukiritimba na unyonyaji," akiongeza kuwa hali hiyo isiyo na usawa "siyo kanuni za maumbile, bali ni kanuni zilizowekwa na watu."

Katika mapendekezo yake muhimu, ripoti hiyo inahimiza kuweka ajenda yenye azma kubwa ya Dunia nzima, kwa kuandika upya kanuni za kodi na biashara za kimataifa ili kuhakikisha kampuni kubwa za kimataifa na ngazi za matajiri zinatoa mchango kwa usawa; kuzifanyia mageuzi sera za nchi ili kusaidia wafanyakazi, kupunguza ulimbikizaji wa utajiri kwa kampuni na kuwekeza katika huduma za umma; na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kodi, biashara na mabadiliko ya kijani wakati huu ambapo hali isiyo tulivu ya siasa za kijiografia inayozidi kuwa mbaya.

Rais Ramaphosa amesema Umoja wa Mataifa tayari umeambiwa kuhusu ripoti hiyo, na kamati yake hiyo itaiwasilisha kwenye Mkutano wa Viongozi wa G20 baadaye mwezi huu.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (wa nne, kulia) akipokea Ripoti ya Kamati Maalum ya G20 juu ya Hali isiyo na Usawa Duniani kutoka kwa Mshindi wa Tuzo ya Nobel Joseph Stiglitz (wa tatu, kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima (wa kwanza, kulia), na wataalamu wengine wanne wakuu wa kimataifa wa kamati hiyo kwenye hafla mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 4, 2025. (Picha na Shakirah Thebus/Xinhua)

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kushoto) akipokea Ripoti ya Kamati Maalum ya G20 juu ya Hali isiyo na Usawa Duniani kutoka kwa Mshindi wa Tuzo ya Nobel Joseph Stiglitz kwenye hafla mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 4, 2025. (Picha na Shakirah Thebus/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha