Lugha Nyingine
Kufungwa kwa serikali ya Marekani kwatarajiwa kuvunja rekodi huku Baraza la Seneti likishindwa tena kupitisha muswada wa bajeti

Picha iliyopigwa Novemba 4, 2025 ikionyesha sehemu ya nje ya Ikulu ya White House, mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)
WASHINGTON – Baraza la Seneti la Bunge la Marekani jana Jumanne limeshindwa tena kupitisha muswada wa bajeti wa muda, na kufikisha jaribio la 14 lisilofanikiwa, ikimaanisha kwamba kufungwa huku kwa serikali kuu ya Marekani kuko kwenye mwelekeo wa kuzidi rekodi ya siku 35 iliyowekwa wakati wa kufungwa kwa serikali mwaka 2018-2019 na kuwa kufungwa kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani.
Baraza hilo la seneti lenye wabunge wengi wa chama cha Republican limepiga kura 54 dhidi ya 44 kuhusu Bunge kuidhinisha “safi” azimio linaloendelea, ambalo lingeipa fedha serikali katika viwango vya sasa hadi Novemba 21. Muswada huo ulihitaji kura 60 ili kushinda kura ya maamuzi na kusonga mbele katika baraza la juu.
Kufungwa huko kwa serikali kunakoendelea kumesababisha usumbufu unaoongezeka, kukiathiri sekta kama vile usafiri wa anga, msaada wa chakula na huduma za afya, huku athari yake ikiendelea kupanuka na kuweka shinikizo kubwa kwa maisha ya watu na uchumi.
Ofisi ya Bajeti ya Baraza imesema katika ripoti yake mpya kuwa hali hiyo inaweza kugharimu uchumi wa Marekani dola bilioni 14 kama itadumu kwa wiki nane zaidi.
Wakati huo huo, vyama viwili vya Republican na Democrats vinaendelea kulaumiana, kila kimoja kikishutumu kingine kwa kusababisha mkwamo huo.
"'Kila siku inakuwa nafuu kwetu.' Hayo yalikuwa maneno ya kiongozi wa wabunge wa chama cha Democrat wiki moja baada ya kufungwa huko kwa serikali, ikionyesha faida zinazodhaniwa za kufungwa huko kwa serikali ya wabunge chama cha Democrat. Lakini kutokana na Wabunge wa Chama cha Democrat, kila siku inazidi kuwa mbaya kwa watu wa Marekani," Kiongozi wa wabunge walio wengi wa Chama cha Republican kwenye Baraza la Seneti John Thune alisema jana Jumanne katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X.
Vituo vya Huduma na Misaada ya Matibabu vimeonya kwamba mara ruzuku iliyoongezwa itakapoisha mwisho wa mwaka, malipo ya wastani ya bima yanaweza kuongezeka kwa takriban asilimia 30 mwaka ujao.
Mpango wa msaada wa chakula unaofuatiliwa sana pia umeathiriwa. Baada ya majaji wawili wa mahakama kuu kuingilia kati, serikali ya Trump ilitangaza Jumatatu wiki hii kwamba itatumia fedha za dharura kudumisha nusu ya manufaa ya Mpango wa Msaada wa Lishe ya Ziada (SNAP) kwa mwezi huu, ikisema kuwa baadhi ya majimbo yanaweza kuchukua wiki au hata miezi kuanza tena usambazaji kamili.
Mpango huo unahusu Wamarekani milioni 42 - takriban moja ya nane ya idadi yote ya watu wa nchi hiyo - ambao wengi wao wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Kura ya maoni ya hivi karibuni ya Gallup imeonyesha kuwa kukubalika kwa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani kumeshuka kwa asilimia 11 hadi asilimia 15 pekee. Kwa sasa, watu wazima karibu wanne kati ya watano wa Marekani -- asilimia 79 -- wanasema hawakubaliani na jinsi Baraza hilo linavyotimiza wajibu wake.

Picha iliyopigwa Novemba 4, 2025 ikionyesha sehemu ya nje ya Ikulu ya White House, mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

Picha iliyopigwa Novemba 4, 2025 ikionyesha sehemu ya nje ya Ikulu ya White House, mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

Watu wanaonekana wakisubiri kupokea chakula cha bila malipo mtaani mjini Portland, Oregon, Marekani, Novemba 4, 2025. (Xinhua/Wu Xiaoling)

Watu wanaonekana wakisubiri kupokea chakula cha bila malipo mtaani mjini Portland, Oregon, Marekani, Novemba 4, 2025. (Xinhua/Wu Xiaoling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



