Rais Xi ahimiza kuimarisha ushirikiano, kuoanisha vema mikakati ya maendeleo na Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 4, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 4, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin jana Jumanne mjini Beijing, akitoa wito wa kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuoanishwa vema kwa mikakati ya maendeleo ya nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, China na Russia zimeyapita bila kuyumbayumba mazingira ya nje yenye misukosuko kwa utulivu mkubwa, zikilenga malengo ya maendeleo ya ngazi ya juu na yenye sifa bora zaidi. Ameongeza kuwa kudumisha, kuimarisha na kusukuma mbele uhusiano wa pande mbili ni chaguo la kimkakati kwa pande zote mbili.

Akisisitiza kuwa dira mpya kwa uhusiano kati ya pande mbili ziliwekwa wakati wa mikutano yake na Rais wa Russia Vladimir Putin mwaka huu, Rais Xi amesema nchi hizo mbili zinapaswa kudumisha uratibu wa karibu, kutekeleza kikamilifu maelewano muhimu ya pamoja yaliyofikiwa na viongozi hao wawili, na kufanyia kazi kupanua keki ya ushirikiano kwa kuzingatia maslahi ya msingi ya nchi hizo mbili na watu wao, ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika amani na maendeleo duniani.

Rais Xi amehimiza juhudi za kupanua bila kuyumba uwekezaji kutoka pande zote na kuimarisha ushirikiano katika nyanja za jadi kama vile nishati, muunganisho wa miundombinu, kilimo na mambo ya anga ya juu, kutumia uwezo bora wa ushirikiano katika sekta mpya kama vile akili mnemba, uchumi wa kidijitali na maendeleo ya kijani ili kukuza vichocheo vipya vya ukuaji kwa ajili ya ushirikiano wa pande mbili.

Amesisitiza kuwa Mapendekezo ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa ajili ya Kuunda Mpango wa 15 wa Miaka Mitano kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii, uliopitishwa kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC, yamefanya muundo wa ngazi ya juu na kuweka dira ya kimkakati kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China katika miaka mitano ijayo.

"China itasukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China kwa njia ya pande zote, kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii yenye sifa bora kwa hatua thabiti, na kupanua ufunguaji mlango wa ngazi ya juu," Rais Xi amesema, akisisitiza kwamba China ina nia ya kushirikiana na Russia ili kuoanisha vema Mpango wake wa 15 wa Miaka Mitano na mikakati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Russia ili kunufaisha watu wa pande zote mbili kila wakati.

Kwa upande wake Mishustin amewasilisha salamu za dhati na za kutakia kila la kheri za Rais Putin kwa mwenzake Xi.

Amesema mikutano miwili kati ya wakuu wa nchi za Russia na China mwaka huu ilipanga kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa pande mbili na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa uratibu wa pande zote kati ya Russia na China.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijin, mji mkuu wa China, Novemba 4, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijin, mji mkuu wa China, Novemba 4, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha