Kiwanda cha mbolea ya kijani kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya China chawekewa jiwe la msingi Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2025

Rais wa Kenya William Ruto akishiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea ya kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Novemba 3, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

NAIROBI – Hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa mradi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kijani unaofadhiliwa na Kundi la Kampuni za Kaishan la China imefanyika jana Jumatatu katika Kaunti ya Nakuru, magharibi-katikati mwa Kenya, ikiashiria hatua kubwa kuelekea kuongeza kwa uendelevu tija ya kilimo cha nchi hiyo.

Kiwanda hicho za kuzalisha mbolea, kinachojengwa kwa ufadhili wa Kundi la Kaishan la China, kitatumia nishati ya mvuke wa jotoardhi inayotolewa na Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Kenya (KenGen). Kiwanda hicho kinakadiriwa kuzalisha megawati 165 za nishati safi ili kutengeneza amonia ya kijani kwa ajili ya uzalishaji wa mwaka wa tani takriban 480,000 za mbolea zisizoleta uchafuzi kwa mazingira.

Rais wa Kenya William Ruto, alishiriki kwenye hafla hiyo, ameisifu jitihada hiyo akiielezea kuwa ni mradi kinara katika mageuzi ya kijani ya viwanda vya Kenya. Amesema kiwanda hicho kipya kitahakikisha wakulima wanapata mbolea za kuaminika, za bei nafuu na zinazozalishwa nchini humo.

"Italinda uchumi wetu kutokana na misukosuko ya bei duniani, kuimarisha hali ya usalama wa chakula na kuokoa fedha za kigeni zenye thamani za nchi ambazo zinaweza kuelekezwa kwenye vipaumbele vingine vya miradi ya nchi ," Ruto amesema.

Rais huyo amesema, mradi huo utaleta nafasi za ajira zaidi ya 2,000, kupunguza bili ya uagizaji mbolea ya Kenya kwa zaidi ya shilingi bilioni 60 (dola za kimarekani karibu milioni 464) kwa mwaka, na kuimarisha nafasi ya nchi hiyo ya kuongoza ukuaji wa kijani na uvumbuzi wa kisasa unaotilia maanani tabianchi barani Afrika.

Tang Yan, meneja mkuu wa Kundi la Kampuni la Kaishan, amesema mradi huo ni mfano wa kujipatia maendeleo endelevu." Tutakamata gesi zisizokuwa nzito kutoka kwenye mvuke wa jotoardhi ili kutoa kaboni dioksidi, ambayo itatumika kwenye kiwanda hicho cha mbolea," amesema.

Tang amesisitiza tena kampuni ya Kundi la Kaishan inajikita katika kuunganisha teknolojia ya nishati ya jotoardhi iliyovumbuliwa na Kundi la Kaishan na rasilimali nyingi za jotoardhi za Kenya kwa kuendeleza nishati ya kijani na maendeleo ya kijani ya viwanda vya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Picha iliyopigwa Novemba 3, 2025 ikionyesha hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

Rais wa Kenya William Ruto akihutubia hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Novemba 3, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

Katibu wa Baraza la Mawaziri la Kenya katika Wizara ya Nishati na Petroli Opiyo Wandayi akishiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Novemba 3, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

Tang Yan, meneja mkuu wa Kundi la Kaishan, akishiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Novemba 3, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

Tang Yan, meneja mkuu wa Kundi la Kaishan, akishiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Novemba 3, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

Picha iliyopigwa Novemba 3, 2025 ikionyesha hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

Picha iliyopigwa Novemba 3, 2025 ikionyesha hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha mbolea za kijani unaofadhiliwa na kampuni ya China iliyofanyika katika Kaunti ya Nakuru, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha