Mlango wa China wafunguliwa zaidi, na fursa za maendeleo kunufaisha dunia nzima

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2025

Mto Huangpu unatiririka kwa mawimbi makubwa, ukivutia macho ya dunia kwa mara nyingine tena. Maonesho ya 8 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China yamepangwa kufunguliwa mjini Shanghai, kesho Jumatano, Novemba 5. Maonyesho hayo makubwa ya biashara duniani, yaliyotolewa, kupendekezwa, kupangwa na kuhimizwa na Rais Xi Jinping, yanaendelea vizuri zaidi siku hadi siku.

Maonesho hayo ya mwaka huu kwa mara nyingine tena yataonyesha kwa dunia kwamba dhamira ya China ya kupanua ufunguaji mlango wa ngazi ya juu, nia yake ya kujitolea katika kuchangia fursa zake za maendeleo na dunia, na dhamira yake ya kuhimiza utandawazi wa kiuchumi duniani kuelekea kuwa wazi, jumuishi, wenye usawa, uwiano na kunufaishana zaidi havitabadilika.

Maonyesho hayo ni dirisha muhimu kwa dunia kuchunguza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na maendeleo ya pamoja duniani. Maonesho hayo ya nane yamevutia nchi, maeneo na mashirika ya kimataifa 155 kushiriki, huku kampuni 4,108 za nje zikionyesha bidhaa zao.

Ukubwa wa jumla wa eneo la maonesho hayo utazidi mita za mraba 430,000 , yakiweka rekodi mpya ya ukubwa wake. Yakiungwa mkono na soko kubwa la zaidi ya watu bilioni 1.4, maonyesho hayo yanajivunia thamani ya jumla ya miamala iliyokusudiwa ya dola za Marekani zaidi ya bilioni 500 katika maonyesho yake ya awamu saba zilizopita. China imedumisha nafasi yake ya kuwa soko la pili kwa ukubwa duniani la kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miaka 16 mfululizo, na idadi yake watu wa kipato cha kati inatarajiwa kuzidi milioni 800 katika muongo ujao.

Maonesho hayo ya mwaka huu ni tukio la kwanza kubwa la diplomasia ya uchumi kuandaliwa na China baada ya Mkutano wa Nne wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ikiyapa umuhimu wa kipekee katika hatua hii maalum. Katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, Pato la Taifa la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mkutano huo uliendelea kuhimiza maendeleo ya sifa bora kama jambo kuu la maendeleo ya uchumi na jamii katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, uliweka mipango muhimu ya kupanua ufunguaji mlango wa ngazi ya juu na kupendekeza kujenga hali mpya ya ushirikiano wa kunufaishana.

Tangu kuanzishwa kwake, Maonyesho hayo yamekuwa yakitoa sera mbalimbali za nafuu na urahisi kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo duniani (LDCs). Mwaka huu, eneo maalum lililokuwepo awali la bidhaa za Afrika limepanuliwa na kuboreshwa zaidi, ili kuhakikisha kampuni na bidhaa kutoka nchi zote zilizoko nyuma kimaendeleo zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, pamoja na nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, zinafurahia vya kutosha utaratibu wa kutotoza ushuru.

Ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea ya kundi la Nchi za Kusini, China siku zote imekuwa mtoaji mchango wa maendeleo duniani na muungaji mkono mkubwa wa ushirikiano wa Kusini na Kusini. Kwa sasa, utaratibu wa uchumi na biashara wa kimataifa umeathiriwa kwa kiasi kikubwa, huku hali ya upande mmoja na kujihami kibiashara vikishamiri. Kadiri hali inavyozidi kuwa ya misukosuko zaidi, ndivyo inavyozidi kuwa muhimu zaidi kudumisha mwelekeo thabiti bila kuyumbayumba.

China inafungua soko lake na kuzidisha ushirikiano, ikitoa msingi imara kwa kampuni kutoka nchi mbalimbali duniani kuunganishwa, zikifanya kazi pamoja na kupanua “keki ya kunufaishana”. Ikikabiliwa na changamoto ya pengo la maendeleo, China inajitahidi kuchukua wajibu wake na kupanua sera yake ya kufungua mlango kwa upande mmoja kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo, kuhimiza kunufaishana fursa kupitia sera za kutotoza ushuru, na kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kunufaishana kiukweli unanufaisha dunia na kuleta manufaa katika siku za baadaye.

Ikikabiliwa na mkondo kinzani wa kujihami kibiashara, China bila kuyumbayumba inaunga mkono mfumo wa biashara wa pande nyingi, inatetea kithabiti haki na maslahi ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza utaratibu wa uchumi na biashara wa kimataifa kuendelezwa kwa mwelekeo wa usawa, jumuishi na mantiki zaidi.

Ukubwa wa taifa uko katika maono yake na uwajibikaji wake. Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China, kama tukio la umma la kimataifa lililopendekezwa na China na kutolewa kwa dunia, yanaonyesha dhamira ya uwajibikaji ya China katika kujenga uchumi wa dunia ulio wazi na kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kunufaishana unanufaisha nchi zote.

Ikikabiliwa na mabadiliko yanayoshika kasi ambayo hayajawahi kuonekana katika karne nzima, China kila wakati imevuka vizuizi kwa fikra pana na kuonesha ufuatiliaji mkubwa kwa mustakabali wa pamoja wa binadamu.

China yenye sera thabiti, uhakika wa ukuaji wa uchumi, na mustakabali mzuri wa maendeleo, inaingiza imani yenye thamani katika dunia yenye mabadiliko. Kwa kutupia macho siku za baadaye katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, China iliyofungua mlango na yenye kujiamini zaidi italeta fursa zaidi za kunufaishana kwa dunia kupitia maendeleo yake ya sifa bora, kujenga kwa pamoja mustakabali bora wa ustawi na maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha