Ushiriki wa Rais wa China katika Mkutano wa viongozi wa APEC unaonesha njia ya ushirikiano wa baadaye wa Asia na Pasifiki

(CRI Online) Novemba 03, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema, ushiriki wa Rais Xi Jinping wa China katika Mkutano wa 32 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Asia-Pasifiki (APEC) na ziara yake ya kiserikali nchini Korea Kusini, vimeonesha njia ya ushirikiano wa baadaye wa Asia na Pasifiki, kuonesha kuwajibika kwa nchi kubwa na kuimarisha urafiki na ujirani mwema.

Bw. Wang Yi amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya ziara hiyo ya Rais Xi iliyomalizika punde nchini Korea Kusini.

Amesema, katika mkutano wa APEC Rais Xi alitoa wito wa kuongeza juhudi za pamoja katika kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi, kujenga mazingira ya uchumi uliofungua mlango katika kanda hiyo, kuiweka minyororo ya viwanda na usambazaji bidhaa katika utulivu na ufanisi, kusukuma mbele mageuzi ya kijani na kidijitali ya biashara, na vilevile kuhimiza maendeleo jumuishi yanayonufaisha wote.

Bw. Wang Yi pia amesema katika ziara yake nchini Korea Kusini, Rais Xi amesisitiza kuwa uchumi wa China utaendelea kutoa fursa nyingi zaidi za maendeleo kwa jumuiya ya biashara duniani, na kwamba kuwekeza China ni sawa na kuwekeza siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha