Rais wa China ahudhuria na kuhutubia Kikao cha kwanza cha Mkutano wa 32 wa viongozi wa APEC

(CRI Online) Oktoba 31, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria leo Ijumaa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 32 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Hwabaek (HICO) huko Gyeongju, Korea Kusini na kutoa hotuba yenye kichwa cha“Kujenga kwa pamoja Uchumi wa Asia na Pasifiki Unaofungua Mlango na Kuwanufaisha Wote.”

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Kwenye hotuba hiyo, Rais Xi amesema, kwa miaka zaidi ya 30 tangu APEC ianzishwe, jumuiya hiyo imekuwa ikiongoza kanda ya Asia na Pasifiki kuibuka katika mstari wa mbele wa maendeleo yaliyofungua mlango duniani, na imeifanya Asia na Pasifiki kuwa eneo lenye nguvu zaidi katika uchumi wa dunia.

Rais Xi alisema, kwa sasa, mabadiliko ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miaka zaidi ya mia moja iliyopita yanatokea kwa kasi kubwa zaidi duniani kote, na kanda ya Asia na Pasifiki inakabiliwa na sintofahamu na mambo ya kuvuruga utulivu katika maendeleo yake, akiongeza kuwa, kadri dhoruba inavyoongezeka, ndivyo pande zote zinatakiwa kushikamana zaidi.

Rais Xi ametoa wito kwa nchi wanachama wa APEC kuendelea kushikilia nia ya awali ya kuanzishwa kwa APEC ya kuhimiza ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu, na kutetea maendeleo ya kufungua mlango ambapo kila mmoja ana fursa na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote. Pia amehimiza juhudi za kusukuma mbele utandawazi wa kiuchumi unaohusisha watu wote na kunufaisha watu wote, na kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki.

Katika hotuba yake hiyo, Rais Xi ametoa mapendekezo matano:

Kwanza, Rais Xi ametoa wito wa juhudi za pamoja za kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi. Pili, rais huyo wa China ametoa wito wa kujenga kwa pamoja mazingira ya uchumi wa kikanda wenye kufungua mlango. Tatu, ametoa wito kwa nchi wanachama wa APEC kufanya kazi pamoja ili kudumisha utulivu na ufanisi wa minyororo ya ugavi na viwanda. Nne, Rais Xi, ametoa wito juu ya kusukuma mbele mageuzi ya kidijitali na kijani katika biashara, na tano, amezihimiza nchi za Asia na Pasifiki kufanya kazi pamoja kuhimiza maendeleo jumuishi na yanayonufaisha wote.

Rais Xi pia amesisitiza kuwa China siku zote inashikilia kithabiti sera ya msingi ya nchi ya kufungua mlango, na imechukua hatua halisi kuhimiza ujenzi wa uchumi wa dunia uliofungua milango.

Huku akibainisha kwamba, mapendekezo kwa ajili ya kuandaa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China yalipitishwa kwenye Mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisiti cha China (CPC), Rais Xi amesema China itatumia fursa hiyo kuzidisha mageuzi kwa kina kwa pande zote, kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kutoa fursa mpya kwa Asia na Pasifiki na dunia kupitia mafanikio mapya ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha