Muungano wa ushirikiano wa vyuo vikuu vya Jiangsu na Afrika waanzishwa Suzhou, China

(CRI Online) Oktoba 28, 2025

Muungano wa ushirikiano wa vyuo vikuu vya Mkoa wa Jiangsu wa China na Afrika umeanzishwa rasmi jana Jumatatu katika Wiki ya Ushirikiano na Mabadilishano ya Kimataifa ya Viwanda-Vyuo Vikuu-Utafiti na Matumizi ya Vyuo Vikuu vya Jiangsu mwaka 2025 iliyoanza Jumatatu katika Chuo Kikuu cha Suzhou, China ikiashiria hatua mpya katika ushirikiano kati ya mkoa wa Jiangsu, China na Afrika.

Muungano huo umezinduliwa kufuatia pendekezo lililotolewa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Viwanda cha Nanjing na Chuo Kiuu cha Johannesburg cha Afrika Kusini, ukijumuisha vyuo vikuu 13 vya mkoa wa Jiangsu na nchi 13 barani Afrika.

Muungano huo utatumika kama "kituo cha kulea" na kuendeleza kwa pamoja vipaji na "kiongeza kasi" kwa ajili ya ushirikiano wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknollojia kati ya China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha