

Lugha Nyingine
Kenya yaanza ujenzi wa kituo cha biashara cha kimataifa ili kuimarisha biashara na China
(Picha/Xinhua)
Rais wa Kenya William Ruto amezindua ujenzi wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha China na Kenya chenye thamani ya shilingi bilioni tano (dola za Kimarekani karibu milioni 38.7), mradi ambao umesanifiwa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya China na Kenya.
Maafisa waandamizi wa serikali, watendaji wa sekta hiyo, na viongozi wa serikali za mitaa walihudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi la kituo hicho cha maonyesho iliyofanyika siku ya Jumatano jijini Nairobi, ambacho kinajengwa na Kampuni ya China Plaza Group.
Ruto amesema mradi huo wa kihistoria wa jengo la matumizi mbalimbali, unaoenea eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zadi ya 68,000, unaonesha imani kubwa katika uchumi wa Kenya kama mazingira thabiti na yanayotabirika ambayo yanazipa faida kampuni na kuhakikisha mapato ya haki kwa wawekezaji.
Kwa mujibu wa Ruto, kituo hicho kitaonesha bidhaa kutoka China vilevile bidhaa zinazotengenezwa Kenya mahsusi kwa ajili ya kusafirishwa kuuzwa kwenye masoko ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma