

Lugha Nyingine
Simulizi za Maendeleo Bora ya Hali ya Juu | Karakana ya Luban: Kufunza vipaji nchini Thailand
Msimulizi: Nitinun Chomchuen (Thailand), Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Tianjin Bohai
Mwaka 2013, Rais Xi Jinping wa China alitoa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. Katika mwaka huohuo, nilipata ufadhili wa masomo wa serikali ya China kwenda kusoma Tianjin.
Baada ya kumaliza masomo yangu ya shahada ya pili mwaka 2016, niliamua kubaki China na kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi cha Tianjin Bohai nikifanya kazi zinazohusiana na mradi wa Karakana ya Luban nchini Thailand.
Mwaka 2016, Chuo cha Ufundi Stadi cha Phra Nakhon Si Ayutthaya cha Thailand na Chuo cha Ufundi Stadi cha Tianjin Bohai kwa pamoja vilianzisha Karakana ya Luban nchini Thailand, karakana ya kwanza ya Luban ya China nje ya nchi. Hadi sasa, karakana hiyo imeshatoa mafunzo kwa wataalamu wa kiufundi zaidi ya 2,000 nchini Thailand na kuunga mkono wanafunzi zaidi ya 460 wa Thailand wanaosoma nchini China.
Ninawajibika zaidi kwa usimamizi wa kila siku wa Karakana ya Luban nchini Thailand, mawasiliano na uratibu kati ya pande za China na Thailand, na kufundisha Kichina wanafunzi wa kimataifa.
Sehemu yenye umuhimu zaidi ya kazi yangu ni kushuhudia ukuaji wa wanafunzi na kukuza urafiki kati ya nchi zetu mbili.
Karakana ya Luban nchini Thailand imepitisha mtindo unaochanganya "elimu ya kitaaluma na mafunzo ya ufundi." Programu zake zote sita za sasa zimefaulu mapitio ya ukaguzi na uidhinishaji wa Kamisheni ya Elimu ya Ufundi ya Wizara ya Elimu ya Thailand.
Wahitimu wa Karakana ya Luban ambao wamesoma katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Tianjin Bohai kama wanafunzi wa kimataifa hutafutwa sana kwenye soko la ajira, kwa sababu wana ubobezi wa hali ya juu wa kiufundi na lugha ya Kichina. Wengi wao huchagua kufanya kazi katika kampuni zinazowekezwa na China nchini Thailand. Mshahara wao kwa ujumla ni wa juu kuliko kiwango cha wastani cha wahitimu wa shule za ufundi za nchini, ambayo inaboresha moja kwa moja hali ya kiuchumi ya wanafunzi na familia zao.
Hii inaonyesha jinsi Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja linavyoboresha maisha ya watu. Kwa mfano, mmoja wa wanafunzi wa kimataifa, Wasan Butsadiwan, anafanya kazi Kampuni ya Haier, Tawi la Thailand. Anavutiwa na uvumbuzi na ubunifu wa Lu Ban. Wakati wa masomo yake kwenye Karakana ya Luban, alipata ujuzi na maarifa mengi, ikiwemo vidhibiti vya mantiki vilivyo katika mifumo ya programu, teknolojia ya roboti na teknolojia ya udhibiti wa nambari za kompyuta. Ujuzi huu wote ni muhimu kwa viwanda vya kisasa.
Karakana ya Luban imetoa suluhisho la China kwa mafunzo ya ujuzi wa kiufundi wa Thailand. Chukua viwanda vya magari yanayotumia nishati mpya kama mfano: Thailand ilianza kwa kuchelewa katika viwanda hivyo na ilikosa uzoefu wa kutosha wa kufundisha. Awamu ya pili ya Karakana ya Luban nchini Thailand ilianzisha kozi ya teknolojia ya magari yanayotumia nishati mpya. Chuo cha Ufundi Stadi cha Tianjin Bohai kilitoa vifaa vya kutosha na kufadhili walimu wa Thailand kupata mafunzo nchini China, ikiwasaidia kufahamu maarifa na teknolojia ya hali ya juu.
BRI ni pendekezo la kubadilisha dunia lililoanzishwa na China ambalo pia limebadilisha maisha yangu. Nilikutana na mume wangu, Jian Peng, kwenye Karakana ya Luban. Sasa sisi ni familia na wenzi.
Katika kipindi cha miaka zaidi ya 12 iliyopita, nimesoma, kufanya kazi na kuishi hapa, nikijenga uhusiano wangu na Karakana ya Luban. Kama nikifanya majumuisho ya uzoefu wangu katika sentensi moja, ninaweza kusema: China na Thailand ni familia!
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma