

Lugha Nyingine
Rais Trump asema Israel imekubali mpango wa Ikulu ya White House kuhusu kusimamisha mapigano Gaza
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2025
![]() |
Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Septemba 29, 2025. (Xinhua/Hu Yousong) |
WASHINGTON - Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekubali mpango wenye vipengele 20 uliopendekezwa na mamlaka ya Trump unaolenga kumaliza mgogoro wa Gaza, kufuatia mazungumzo yao katika Ikulu ya White House jana Jumatatu.
"Pia ninataka kumshukuru Waziri Mkuu Netanyahu kwa kukubaliana na mpango huo na kwa kuamini kwamba kama tutafanya kazi pamoja, tunaweza kufikisha mwisho vifo na uharibifu ambao tumekuwa tukiuona kwa miaka, miongo, hata karne nyingi, na kuanza ukurasa mpya wa usalama, amani na ustawi kwa kanda zima," Trump amesema kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House.
Trump pia ametoa wito kwa Hamas kukubali masharti ya pendekezo hilo la amani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma