

Lugha Nyingine
Simulizi za Maendeleo Bora ya Hali ya Juu | Mafungamano ya mambo ya kifedha yawasha taa za nyumba katika "Nchi ya Upinde wa Mvua"
Msimulizi: Shen Hua, Meneja Mkuu, Idara ya Biashara ya Mambo ya Fedha, Tawi la Johannesburg la Benki ya China
Afrika Kusini kwa muda mrefu imekuwa ikisumbuliwa na uhaba wa umeme. Ili kukabiliana na tatizo hilo la umeme, serikali ya Afrika Kusini imekuwa ikijitahidi kuendeleza nishati mbadala katika miaka ya hivi karibuni. Mwaka 2024, kufuatia wito wa zabuni kutoka kwa serikali ya Afrika Kusini, Kampuni ya PowerChina ilitia saini mkataba wa miradi ya mifumo ya kuhifadhi nishati ya betri ya Oasis 1. Mara miradi hiyo itakapokamilika, itahifadhi MWh 1,000 za umeme, zinazotosha kukidhi mahitaji ya nishati ya nyumba za familia 100,000 kwa siku. Miradi hii itawasha nyumba za famillia katika "Nchi ya Upinde wa Mvua".
Mmiliki wa miradi hiyo ya mifumo ya kuhifadhi nishati ya betri ya Oasis 1 ni Electricite De France (EDF), kampuni iliyowekezwa na mtaji wa kigeni ambayo inashikilia nafasi kubwa katika soko la nishati la Afrika Kusini. Kwa muda mrefu, ilikuwa karibu haiwezekani kwa kampuni za China kushiriki katika miradi ya nishati kama hii nchini Afrika Kusini.
Sababu ni ya kiutendaji: kwa upande mmoja, kampuni za Ulaya na Marekani zina mizizi mirefu katika sekta ya nishati ya Afrika Kusini; kwa upande mwingine, baadhi ya taasisi za fedha za kimataifa hazina uelewa wa mitindo ya biashara ya kampuni za China na miundo ya mambo ya fedha. Hii ni kweli hasa kwa miradi ya mali nyepesi inayojikita katika vifaa na ufungaji, ambapo ni vigumu kupata mkopo kutoka kwa benki za nchi husika.
Lakini wakati huu, hali imebadilika. Kuteuliwa kwa kampuni hiyo ya PowerChina kuwa mkandarasi kulitegemea ufadhili wa kifedha kutoka Benki ya China. Benki hiyo inafanya kazi kama mdhamini wa mkopo, ikitoa udhamini unaofuata kanuni za soko la Afrika Kusini ili kuhakikisha utekelezaji kamilifu wa mkataba wa PowerChina. Hii inasaidia kampuni kushinda vizuizi vya kuingia kwa kuhakikisha wakandarasi wanaweza kupokea malipo ya mapema na kuendelea na ujenzi huku ikipunguza hatari kwa wamiliki wa miradi na kuimarisha taswira ya kitaaluma ya kampuni za China katika miradi ya kimataifa.
Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kutia saini vyaraka za ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) na China. Maendeleo ya kijani ni sifa ya kipekee ya BRI, na maendeleo ya kijani na ushirikiano wa nishati ni maeneo muhimu kwa uungaji mkono wa Benki ya China nchini Afrika Kusini.
Mwaka 2022, Benki ya China tawi la Johannesburg ilitoa hati fungani ya kwanza barani Afrika inayoongozwa na benki ya nchini China, ikipata dola milioni 300 za Kimarekani. Mwaka 2024, benki hiyo ilitoa yuan milioni 30 (Dola za Kimarekani karibu Milioni 4.1) katika ufadhili kwa Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la Serikali ya China Tawi la Afrika Kusini kuunga mkono upanuzi wa barabara kuu mjini Durban. Mwezi Julai, Benki ya China ilifikia makubaliano na kiwanda cha BAIC cha Afrika Kusini kuunga mkono mradi wake wa magari ya nishati mpya.
Mafungamano ya mambo ya fedha yanatoa uungaji mkono muhimu kwa kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja. Kila ufadhili hutumika kama msukumo wa kugeuza ushirikiano wa BRI kati ya China na Afrika Kusini kutoka maono hadi uhalisia, ikitoa mchango kwa ajili ya kuendana kati ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Mpango wa Kujenga Upya na Kuimarisha Uchumi wa Afrika Kusini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma