Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa DPRK

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Choe Son Hui mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 28, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Choe Son Hui mjini Beijing jana Jumapili, akisema kuwa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa pande mbili muda wote imekuwa mwongozo thabiti wa kimkakati wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali ya China.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, amesema China na DPRK ni majirani rafiki ambao wameunganishwa na milima na mito, akiongeza kuwa urafiki wa jadi ulioanzishwa na kukuzwa na vizazi vikongwe vya viongozi wa vyama na nchi hizo mbili ni mali yenye thamani ya pande zote mbili.

“Mapema mwezi huu, Katibu Mkuu Xi Jinping na Katibu Mkuu Kim Jong Un walifanya mkutano wa kihistoria na kufikia makubaliano muhimu, wakionyesha mwelekeo na kuweka dira kwa maendeleo ya uhusiano wa China na DPRK,” Wang amebainisha.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa vyama na nchi hizo mbili, kuboresha mawasiliano ya kimkakati na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, ili kuboresha zaidi ustawi wa watu wa nchi hizo mbili na kwa pamoja kuhimiza amani na maendeleo ya kikanda.

Wang pia amefahamisha hali ya ndani ya China, akisema kuwa kwa kuwa China na DPRK ni nchi za kijamaa zenye maadili na malengo ya pamoja, pande hizo mbili zinapaswa kuongeza mawasiliano ya uzoefu katika usimamizi na utawala ili kuhimiza maendeleo ya mambo yao ya kijamaa.

Wang amesema kuwa China inathamini uungaji mkono thabiti wa DPRK kwa maslahi makuu na yale yanayofuatiliwa na China, vilevile uungaji wake mkono kwa dhana ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na Pendekezo la Maendeleo Duniani, Pendekezo la Usalama Duniani, Pendekezo la Ustaarabu Duniani, na Pendekezo la Usimamizi Duniani yaliyopendekezwa na China.

"China inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na DPRK katika masuala ya kimataifa na kikanda, kupinga aina zote za umwamba, na kulinda maslahi ya pamoja ya pande zote mbili na haki na usawa wa kimataifa," ameongeza.

Kwa upande wake Choe amesema, Shughuli za China za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti vimedhihirisha kikamilifu mafanikio ya kihistoria, nguvu kamili ya taifa na hadhi ya kimataifa ya China.

"Mkutano wa kihistoria uliofanywa na viongozi wakuu wa vyama na nchi hizo mbili umetoa mwongozo wa kimkakati na msukumo mkubwa wa kuzidisha uhusiano kati ya DPRK na China," Choe ameongeza.

Choe pia amesema DPRK inapenda kushirikiana kwa karibu na China katika masuala ya pande nyingi, kwa pamoja kupinga msimamo wa upande mmoja na siasa za nguvu, na kuhimiza utaratibu wa dunia ulio wa haki na usawa zaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Choe Son Hui mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 28, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Choe Son Hui mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 28, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha