Kutoka mtazamaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing hadi mshiriki wa ujenzi wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2025

Mwaka 2010, nikichochewa na ndoto ya utotoni, nilikanyaga ardhi ya China. Yote yalichochewa na tukio la kushangaza la Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Beijing mwaka 2008. Siku yangu ya kuzaliwa ilikuwa Agosti 8, na katika siku hiyo ya mwaka 2008, nilishuhudia kuwashwa kwa mwenge wa Olimpiki kwenye runinga, na China imekuwa ikikumbukwa nami moyoni tangu wakati huo.

Mwaka 2021, nilianza kufanya shughuli zangu katika mji wa Xi'an wa China kwa sababu ni kituo muhimu cha Reli ya Uchukuzi wa Haraka ya China-Ulaya. Reli hiyo (Upande wa Xi'an) inaongoza China kwa safari za treni kwa mwaka, ikiunganisha kwa ufanisi vituo vikuu vya Asia ya Kati na Ulaya. Aidha, uungaji mkono wa kisera na huduma bora za Eneo la Bandari ya Kimataifa ya Xi'an vinafanya kuwa rahisi kwa kampuni chipukizi kuanza safari hii.

Reli ya Uchukuzi wa Haraka ya China-Ulaya imekuwa kichocheo kikuu cha maendeleo ya biashara yangu. Sisi ni kampuni ya kimataifa inayojikita mahsusi katika uchukuzi wa makontena wa kuvuka mpaka kati ya Asia na Ulaya. Kuongezeka kwa idadi ya safari na uendeshaji tulivu wa Reli hiyo kumebadilisha mantiki ya uchukuzi wa biashara ya kati ya Asia na Ulaya, kwa gharama robo tu ya uchukuzi mizigo kwa anga na muda wa theluthi mbili kuliko uchukuzi wa baharini.

Kwa sasa, kampuni inashughulikia treni takriban 100 za kuagiza na kuuza bidhaa nje kila mwezi. Kuanzia mahitaji ya kila siku na vifaa vya nyumbani vya kutumia umeme hadi magari yenye kutumia nishati mpya, tunaweza kuwasilisha bidhaa kituo-hadi-kituo kwa wateja duniani kote. Tunapelekea maeneo mengine uzoefu wenye mafanikio wa Xi'an: tawi tayari limeanzishwa mjini Qingdao, huku matawi mjini Shanghai na Chengdu pia yakiwa yamepangwa.

Usafiri bila Visa, safari za moja kwa moja za ndege na malipo ya kuvuka mpaka hurahisisha usafiri kati ya Kazakhstan na China, na kuufanya uwe rahisi kama majirani wanaotembelea. Hii si tu inaongeza matumizi ya utalii na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, lakini pia inaonyesha mafanikio ya pamoja ya nchi hizo mbili katika kujenga kwa pamoja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Kutoka Astana hadi Xi'an, nimepitia kutoka kuwa mtazamaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing hadi mshiriki wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. Usalama, hamasa, na ujumuishi wa mahali hapa vimeniruhusu kukita mizizi zaidi na zaidi. China si soko tu; ni udongo wenye rutuba kwa ndoto.

(Ilisimuliwa na Nursulu Zholbaskanova, Mkazakhstan, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uchukuzi wa Kimataifa ya TERRAcont iliyopo Xi'an, na kuandikwa na waandishi wa habari wa People's Daily Online Zhang Lulu na Cui Yue)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha