China yatajwa kuongoza soko la roboti za viwanda duniani ikiwa na ufungaji wenye kuvunja rekodi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2025

Mtembeleaji maonyesho akiwasiliana na roboti kwenye Baraza la Uvumbuzi la Pujiang 2025 lililofanyika mjini Shanghai, mashariki mwa China, Septemba 21, 2025. (Xinhua/Fang Zhe)

Mtembeleaji maonyesho akiwasiliana na roboti kwenye Baraza la Uvumbuzi la Pujiang 2025 lililofanyika mjini Shanghai, mashariki mwa China, Septemba 21, 2025. (Xinhua/Fang Zhe)

BERLIN – Idadi ya roboti za viwandani nchini China ilifikia rekodi ya roboti 2,027,000 mwaka 2024, ikichukua zaidi ya nusu ya mahitaji ya duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Roboti Duniani 2025 iliyotolewa jana Alhamisi na Shirikisho la Kimataifa la Roboti (IFR) lenye makao yake mjini Frankfurt, Ujerumani.

Ufungaji roboti kwa mwaka nchini China ulipanda hadi roboti 295,000, ongezeko la asilimia 7 kutoka mwaka 2023, ikimaanisha kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa, ripoti hiyo imesema.

Imeeleza kuwa, roboti 542,000 za viwandani zilifungwa mwaka 2024 kote duniani, zaidi ya mara mbili ya idadi ya muongo mmoja uliopita, na ufungaji roboti duniani ulizidi roboti 500,000 kwa mwaka wa nne mfululizo.

"Mkakati wa China wa kuufanya viwanda hivyo kuwa vya kisasa umefikia hatua mpya katika msukumo wa nchi hiyo kwa mambo ya otomatiki," Rais wa IFR Takayuki Ito amesema.

"Idadi ya roboti iliongezeka maradufu ndani ya miaka mitatu, ikizidi roboti milioni 1 mwaka 2021 na sasa ikihesabu roboti milioni 2 mwaka 2024" ameongeza.

Bara la Asia limebaki kuwa soko kuu, likichukua asilimia 74 ya matumizi mapya ya roboti mwaka 2024, ikilinganishwa na asilimia 16 barani Ulaya na asilimia 9 katika nchi za Amerika.

Roboti ikifanya maonyesho kwenye hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Tatu ya Ufundi Stadi mjini Zhengzhou, Mkoani Henan, katikati mwa China, Septemba 19, 2025. (Xinhua/Hao Yuan)

Roboti ikifanya maonyesho kwenye hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Tatu ya Ufundi Stadi mjini Zhengzhou, Mkoani Henan, katikati mwa China, Septemba 19, 2025. (Xinhua/Hao Yuan)

Nchini China, sekta za umeme na elektroniki zimeendelea kuongoza kwa mahitaji huku vifaa 83,000 vikiwa vilifungwa mwaka 2024, ikifuatiwa na sekta ya magari kwa kufungwa kwa vifaa 57,200. Wauzaji wa ndani pia walipanua uwepo wao katika usindikaji chakula, nguo na bidhaa za mbao.

Kwa mara ya kwanza, kampuni za China za kuunda roboti ziliuza roboti nyingi zaidi nchini kuliko washindani wa kigeni, huku soko lao la ndani likipanda hadi asilimia 57 mwaka 2024 kutoka asilimia 47 mwaka 2023, ripoti hiyo imesema. Utafiti wa IFR wa robo ya kwanza ya 2025 pia ulionyesha ukuaji mkubwa wa tarakimu mbili katika oda za roboti kote Asia, ukisababishwa zaidi na China.

Duniani kote, jumla ya idadi ya roboti za viwandani zinazofanya kazi ilifikia roboti 4,664,000 mwaka 2024, ongezeko la asilimia 9 kutoka mwaka uliopita.

Ito amesema kuwa ingawa hali ya uchumi mkuu duniani inaweza kusababisha changamoto ya muda mfupi, mwelekeo wa ukuaji wa muda mrefu unabaki kuwa imara.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa viwanda vya roboti duniani vitadumisha ukuaji thabiti. Duniani kote ufungaji roboti unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 6 hadi kufikia roboti 575,000 mwaka 2025 na kuzidi roboti 700,000 ifikapo mwaka 2028, huku kukiwa na ukuaji wa wastani kwa mwaka wa karibu asilimia 10 hadi wakati huo. China inatarajiwa kuendelea kuwa soko kubwa zaidi duniani kupita kipindi hicho.

Roboti akionyesha ustadi wa kuepuka vizuizi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Nanning mjini Nanning, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, China, Septemba 19, 2025. (Xinhua/Zhang Ailin)

Roboti akionyesha ustadi wa kuepuka vizuizi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Nanning mjini Nanning, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, China, Septemba 19, 2025. (Xinhua/Zhang Ailin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha