Lugha Nyingine
Wanafunzi wa Namibia waanza safari kuelekea China kwa mafunzo kuhusu nishati ya nyuklia na utamaduni
Kundi la wanafunzi 12 wa Namibia wenye umri kati ya miaka 13 na 16 wameondoka mwishoni mwa wiki siku ya Jumamosi kwa ziara ya siku 10 nchini China inayolenga kuwapa ujuzi wa uvumbuzi wa kisayansi na mafunzo kuhusu utamaduni chini ya programu inayoitwa “Nishati ya Nyuklia yaangazia Ndoto, Urafiki wajenga Kesho.”
Programu hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Rossing Uranium, iliyonunuliwa na kampuni ya madini ya Namibia ya Shirika la Nishati ya Nyuklia na Uranium la China (CNUC).
Lengo la programu hiyo ni kuwafahamisha wanafunzi hao maendeleo ya sayansi na teknolojia, na kuhimiza maelewano kati ya nchi hizo mbili.
Kwenye hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika mjini Windhoek, wanafunzi walionyesha furaha yao kuhusu ziara hiyo itakayowafikisha kwenye miji kadhaa ya China ikiwemo ya Beijing, Tongliao, Zhangzhou, na Xiamen.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



