Lugha Nyingine
Guinea-Bissau yaunga mkono pendekezo la China kuhusu usimamizi wa dunia
(CRI Online) Septemba 19, 2025
Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo amesema, nchi hiyo inaunga mkono pendekezo la China kuhusu usimamizi wa dunia, na iko tayari kutoa mchango katika kujenga mfumo wa usimamizi wa dunia ulio na haki zaidi.
Rais Embalo amesema hayo alipofanya mazungumzo na Balozi wa China nchini humo Yang Renhuo. Pia amesema Guinea-Bissau inapenda kushirikiana na China kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kukuza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati.
Kwa upande wake Balozi Yang amesema, China inapenda kushirikiana na nchi za Dunia ya Kusini ikiwemo Guinea-Bissau, ili kusukuma mbele utekelezaji wa pendekezo hilo na kushirikiana na kuelekea jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



