Lugha Nyingine
China yasema mapendekezo manne ya kimataifa yanaendana na malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian jana amesema, Mapendekezo manne ya kimataifa yaliyotolewa na China yanaendana na malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, na yataingiza nguvu chanya kwa dunia inayokabiliwa na migogoro na mabadiliko, na kutoa msukumo mkubwa kwa maendeleo ya binadamu.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alisema kuwa mapendekezo ya kimataifa yaliyotolewa na China yanaendana na Katiba ya Umoja wa Mataifa, yanaheshimu msimamo wa pande nyingi, yanaunga mkono Umoja wa Mataifa kuwa kiongozi wa mashirika ya kimataifa, na yanaunga mkono kwa nguvu zote hadhi kuu ya Umoja wa Mataifa likiwa shirika la pande nyingi, na kujikita katika kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na kutatua migogoro kwa amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



