

Lugha Nyingine
Ukuaji wa GDP wa taasisi ya fedha Afrika Magharibi washuka na kufikia asilimia 6.5 katika nusu ya pili ya mwaka
Ukuaji wa jumla wa Pato la Ndani katika kanda ya Umoja wa Uchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (UEMOA) umeshuka katika nusu ya pili ya mwaka 2025, na kupungua kutoka asilimia 7 hadi asilimia 6.5.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 3 wa Kamati ya Sera za Kifedha, uliofanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, Gavana wa Benki Kuu za Nchi za Afrika Magharibi (BCEAO) Jean-Claude Kassi Brou amesema, kiwango halisi cha ukuaji katika kanda hiyo kimesalia kuwa asilimia 6.5 katika nusu ya pili ya mwaka, ikiwa ni chini kidogo ya asilimia 7 iliyorekodiwa katika nusu ya kwanza ya mwaka.
Amesema kiwango cha ongezeko la gharama ya maisha katika kanda hiyo kimeendelea kushuka na kufikia asilimia 0.6 katika nusu ya pili ya mwaka kutokana na hatua kadhaa, ikiwemo kuboresha upatikanaji wa bidhaa za chakula za huko, gharama ndogo ya bidhaa za chakula zinaoagizwa kutoka nje, na kushuka kwa bei ya mafuta katika baadhi ya nchi za Umoja huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma