Sekta ya usafiri wa anga Tanzania Zanzibar yarekodi ukuaji wa kasi

(CRI Online) Septemba 18, 2025

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) Seif Abdallah Juma amesema, sekta ya viwanja vya ndege visiwani humo imerekodi ukuaji mkubwa katika miaka mitano iliyopita.

Akizungumza na wanahabari hapo jana, Juma amesema Mamlaka hiyo imetimiza maboresho katika miundombinu ya viwanja vya ndege na huduma zake, ikiungwa mkono na sera nzuri na ufadhili wa serikali. Amesema idadi ya abiria iliongezeka kutoka 840,599 mwaka 2020 hadi milioni 2.4 mwaka jana, huku matarajio yakiwa ni kuzidi abiria milioni 2.8 mwaka huu.

Pia amesema Mamlaka yake imepokea tuzo mbalimbali za kimataifa, ikiwemo tuzo ya kutambuliwa kutoka Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege na hati ya RA3 ya Umoja wa Ulaya kwa usalama wa mizigo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha