

Lugha Nyingine
UM watoa mafunzo kwa maofisa wa Somalia na Umoja wa Afrika kuimarisha usalama wa usafiri wa anga
(CRI Online) Septemba 18, 2025
Ofisi ya Usaidizi wa Operesheni za Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) imesema, maofisa 21 wa usafiri wa anga wamemaliza mafunzo maalum yatakayowawezesha kukabiliana kwa ufanisi na dharura za usafiri wa anga katika viwanja vya ndege na kambi muhimu zinazotumiwa nchini Somalia.
Ofisi hiyo imesema Mafunzo ya Uokoaji na Zimamoto yamewawezesha washiriki kuwa na ujuzi unaotakiwa kushughulikia matukio ya angani na kulinda maisha nchini Somalia.
Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia hapo jana, mkuu wa huduma za usafiri wa anga katika Ofisi hiyo Ernest Manzano amesema, lengo ni kujenga uwezo na kutoa ujuzi wa kipekee kwa raia wa Somalia, kuwawezesha kuchukua majukumu hayo muhimu na kukidhi vigezo vya kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma