

Lugha Nyingine
Marekani kuongeza ushuru wa ziada wa 25% kwa bidhaa zinazotoka India
Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya utendaji jana, na kuweka ushuru wa ziada wa 25% kwa bidhaa zinazotoka India, kutokana na India kuagiza mafuta ya petroli kutoka Russia kwa njia ya moja kwa moja ama isiyo ya moja kwa moja.
Hatua hii inamaanisha kwamba, kiwango cha jumla cha ushuru wa Marekani kwa India kitafikia 50%.
Kulingana na taarifa ya Ikulu ya Marekani iliyotolewa jana, rais Trump amesema hatua na sera za serikali ya Russia zinaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa wa Marekanii, na kwamba kuweka ushuru wa ziada kwa India ni hatua ya lazima na inayofaa ili kushughulikia dharura ya kitaifa iliyosababishwa na mzozo wa Russia na Ukraine.
Taarifa hiyo imesema, ushuru huo mpya utaanza kutumika siku 21 baada ya amri ya utendaji kutolewa, isipokuwa kwa baadhi ya bidhaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma