Kinywaji cha chai ya Zhenzhu ya China chajulikana kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2025

Katika miaka ya hivi karibuni, vinywaji vya aina mpya za chai ya China vyenye ladha mbalimbali, vinavyotokana na mchanganyiko wa vionjo mbalimbali kama vile matunda freshi, majani ya chai, maziwa na jibini, vimepanua soko lake kwa haraka, na kuvutia wateja wa China na nchi za nje.

Takwimu za utafiti uliofanywa na kampuni ya iiMedia zinaonyesha kuwa, mwaka 2024 thamani ya soko la vinywaji vya chai ya mtindo mpya nchini China ilikuwa zaidi ya Yuan bilioni 350 (sawa na dola za kimarekani bilioni 48.5) -- likiwa ni ongezeko la asilimia 6.4 kuliko mwaka 2023 , huku thamani ya soko ikitarajiwa kufikia yuan bilioni 374.93 mwishoni mwa mwaka 2025.

Picha hii iliyopigwa Julai 15 2025 inaonyesha duka la CHAGEE, linalouza chai ya China chapa ya Zhenzhu, huko Jakarta, Indonesia. (Xinhua/Feng Yulin)

Picha hii iliyopigwa Julai 15 2025 inaonyesha duka la CHAGEE, linalouza chai ya China chapa ya Zhenzhu, huko Jakarta, Indonesia. (Xinhua/Feng Yulin)

Ripoti iliyotolewa na gazeti la Nanfang Metropolis Daily inasema chapa za kinywaji cha chai za mtindo mpya wa China zilianza kufungua maduka nje ya nchi katika miaka ya 2010 kwa kasi. Kwa mujibu wa gazeti la Business National Daily, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, chapa za vinywaji vya chai za China zilifungua zaidi ya maduka 5,000 nje ya nchi.

Wakati vinywaji mbalimbali vya chai ya mtindo mpya ya China vikiwa vinaonekana katika miji mingi ya Magharibi kama vile London na Sydney, Asia ya Kusini-Mashariki iliibuka kama moja ya masoko yao kuu.

HEYTEA, ambayo inajivunia kuwa na maduka zaidi ya 4,000 duniani kote, ilifungua duka lake la kwanza nje ya nchi katika Singapore mwaka wa 2018. Naixue ilifungua duka lake la kwanza nje ya nchi mwaka jana katika kituo maarufu cha manunuzi cha Bangkok Central World, na hivyo kuzusha ufuatiliaji mkubwa miongoni mwa wateja vijana.

Chen Fuqiao, mtafiti mshiriki wa Chuo cha Sayansi ya Kilimo cha China (CAAS), amesema umaarufu wa vinywaji vya aina mpya ya chai ya China unaonyesha matarajio ya watu, hasa vijana, wanaopenda vinywaji vya kusaidia afya na kupunguza hisia mbaya.

Picha hii ya kumbukumbu inaonyesha watu kwenye foleni katika duka la Mixue, linalouza chai ya China chapa ya Zhenzhu, huko Sydney, Australia. (Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu inaonyesha watu kwenye foleni katika duka la Mixue, linalouza chai ya Zhenzhu  ya China, huko Sydney, Australia. (Xinhua)

Watu wanaonja aina mpya ya vinywaji vya chai kwenye mgahawa wa chai katika  Eneo la Tunxi la  Mji Huangshan, Mkoani Anhui, China, tarehe 15 Julai 2025. (Xinhua/Cao Li)

Watu wanaonja aina mpya ya vinywaji vya chai kwenye mgahawa wa chai katika Eneo la Tunxi la Mji Huangshan, Mkoani Anhui, China, tarehe 15 Julai 2025. (Xinhua/Cao Li)

Wafanyakazi wanatengeneza vinywaji vya chai ya mtindo mpya kwenye mgahawa wa chai katika  Eneo la Tunxi la  Mji Huangshan, Mkoani Anhui, China, tarehe 15 Julai 2025. (Xinhua/Cao Li)

Wafanyakazi wanatengeneza vinywaji vya chai ya mtindo mpya kwenye mgahawa wa chai katika Eneo la Tunxi la Mji Huangshan, Mkoani Anhui, China, tarehe 15 Julai 2025. (Xinhua/Cao Li)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha