Beijing yajiandaa kwa ajili ya Mkutano wa Roboti wa Dunia wa 2025 na uvumbuzi wa roboti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 04, 2025
Beijing yajiandaa kwa ajili ya Mkutano wa Roboti wa Dunia wa 2025 na uvumbuzi wa roboti
Roboti yenye umbo la binadamu ikiwa kwenye mkutano wa Roboti wa Dunia wa mwaka 2024 mjini Beijing, Agosti 21, 2024. (Xinhua/Ren Chao)

Zaidi ya bidhaa 100 za kisasa za roboti zitaonyeshwa kwenye maonyesho ya kwanza ya Mkutano ujao wa Roboti wa Dunia wa mwaka 2025 utakaofanyika mjini Beijing, zikiwa karibu mara mbili ya bidhaa zilizoonyeshwa mwaka jana, na kuonyesha kupanda ngazi kwa mkutano huo kama jukwaa la kimataifa la uvumbuzi.

Mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 8 hadi 12 Agosti katika Eneo la Maendeleo ya Uchumi na Teknolojia ya Beijing, ambalo pia linajulikana kama Beijing E-Town, chini ya kauli mbiu ya “Kufanya Roboti Kuwa teknolojia za kisasa, na kuwa na akili zaidi”. Kwenye mkutano huo kutakuwa na maonyesho zaidi ya 1,500 kutoka kwa makampuni zaidi ya 200 ya roboti kutoka duniani kote.

Kipengele muhimu kitakuwa ni kuoneshwa kwa mara ya kwanza kwa bidhaa za kisasa, kuanzia roboti za kisasa zenye unyumbufu, roboti za uokoaji, na roboti za ukaguzi hadi roboti za kisasa zinazounda katheta na roboti za mashine za kukata nyasi, zitazowaonyesha watu watakaohudhuria mkutano wa roboti za siku zijazo.

Roboti za binadamu ndio kivutio kikubwa cha mkutano huo, huku watengenezaji 50 wa roboti zenye mwili kamili wa binadamu wakionyesha ubunifu wao wa hivi karibuni.

Mwaka 2024, China ilituma theluthi mbili ya maombi ya haki miliki za roboti , ikatoa roboti 556,000 za viwandani, na kuwa mtengenezaji mkubwa zaidi wa robot duniani. Mkuu wa Taasisi ya mambo ya Elektroniki ya China Xu, Xiaolan, amesema katika muongo mmoja uliopita, idadi ya taasisi kimataifa zinazounga mkono mkutano huo imeongezeka kutoka 12 hadi 28, wakati washiriki kutoka nje wameongezeka kutoka zaidi ya 10 hadi zaidi ya 80.

Mkutano wa mwaka huu unaoratibiwa na Taasisi ya Elektroniki ya China na Shirika la Ushirikiano wa Roboti Duniani, na unatarajiwa kuvutia idadi kubwa ya taasisi za kimataifa. Tamasha la watumiaji wa roboti pia litaendeshwa wakati mmoja na mkutano huo, unaolenga kuimarisha uboreshaji wa roboti za viwanda na mahitaji ya watumiaji.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha