

Lugha Nyingine
Rwanda yaidhinisha makubaliano ya amani na DRC
KIGALI - Rwanda imepitiasha Jumatano jioni wiki hii mswada wa sheria ambayo inaidhinisha makubaliano ya amani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyosainiwa mjini Washington, D.C. Juni 27, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Rwanda.
Makubaliano hayo ni hatua muhimu katika kushughulikia masuala ya usalama yanayofuatiliwa na Rwanda, kurejesha amani na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu, na kuhimiza utandawazi wa kiuchumi ya kikanda, inasomeka taarifa hiyo.
"Rwanda inaendelea kufanya juhudi kwenye utekelezaji wa makubaliano hayo na inatazamia kuhitimishwa kwa Mazungumzo ya Doha, yanayowezeshwa na Nchi ya Qatar kwa uungaji mkono wa Umoja wa Afrika," imeongeza.
Makubaliano hayo ya kina ya amani, ambayo yalianza kutekelezwa mara tu baada ya kutiwa saini, yanaeleza kuanzishwa kwa utaratibu wa pamoja wa kuratibu masuala ya usalama ndani ya siku 30. Pia yanajumuisha ahadi za kuheshimu ukamilifu wa ardhi, kusitisha uhasama, kutoshambuliana na kunyang'anya silaha vikosi vya kijeshi, na kujumuisha kwa masharti makundi yenye silaha yasiyo ya serikali.
Makubaliano hayo pia yana vifungu kuhusu kuwezesha wakimbizi na watu wanaopoteza makazi yao ndani kurejesha nyumbani kwa usalama na kwa hiari, kusisitiza tena jukumu la kulinda amani la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Utulivu nchini DRC, na kuhimiza mafungamano ya kikanda kupitia mipango ya maendeleo ya kuvuka mpaka.
Kwa miongo kadhaa, eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likikumbwa na ghasia, hali iliyokuwa mbaya zaidi na kuibuka tena kwa Kundi la M23 tangu mwishoni mwa mwaka 2021. Kinshasa inaishutumu Kigali kwa kuunga mkono kundi hilo la waasi, madai ambayo yamekuwa yakikataliwa na mamlaka za Rwanda.
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma