Rais Trump agunduliwa kuwa na tatizo la “kupungua uwezo wa mishipa ya damu"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2025

Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akijibu maswali kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Julai 17, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amegunduliwa kuwa na tatizo la kawaida na lisilo na madhara makubwa kiafya la mshipa baada ya kupata uvimbe kwenye sehemu za chini za miguu yake, Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt ametangaza jana Alhamisi ambapo amesema, matokeo ya vipimo vya ultrasound vilivyofanywa kwenye miguu ya Trump yameonyesha kupungua uwezo wa mishipa ya damu, hali ambayo hupatikana mara kwa mara kwa watu wenye umri wa miaka zaidi ya 70.

Leavitt amesema matokeo ya vipimo vya ziada yamemuonyesha Trump "hana dalili za kushindwa kwa moyo, kuharibika kwa figo au ugonjwa wa kimfumo."

Trump, mwenye umri wa miaka 79, alipigwa picha hivi karibuni kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025 mjini East Rutherford, New Jersey, ambapo uvimbe ulioonekana kwenye vifundo vyake vya mguu ulizua uvumi kuhusu afya yake. 

Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akijibu maswali kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Julai 17, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akijibu maswali kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Julai 17, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha