China siku zote imekuwa ikichukua hatua madhubuti kuendeleza maendeleo ya kimataifa: Msemaji

(CRI Online) Julai 18, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China siku zote imekuwa nchi inayochukua hatua madhubuti katika kuendeleza maendeleo ya kimataifa, na inapenda kushirikiana na pande zote kuhimiza ustawi na maendeleo ya pamoja duniani.

Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Alhamisi mjini Beijing, Bw. Lin amesema, janga la maendeleo limekuwa ni changamoto halisi inayozikabili nchi zote, na China siku zote imekuwa ikichukua hatua thabiti kuendeleza maendeleo ya kimataifa.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ya tathmini ya utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030, ikionyesha kuwa karibu nusu ya malengo yamepiga hatua polepole, na asilimia 18 ya malengo yamerudi nyuma.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, dunia inakabiliwa na "dharura ya maendeleo", lakini malengo hayo bado yanaweza kufikiwa, endapo pande zote zinaweza kuchukua hatua za haraka, za pamoja na zisizo za kuyumbayumba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha