Peng Liyuan ashiriki kwenye shughuli ya Uhusiano na Kuliang: Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2025

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, akishiriki kwenye shughuli ya Uhusiano na Kuliang: Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025 na kutoa hotuba katika  Shirika la Urafiki wa Watu wa China na Nchi za Nje  tarehe 17 Julai 2025. (Xinhua/Gao Jie)

BEIJING - Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, jana Alhamisi alishiriki kwenye shughuli ya Uhusiano na Kuliang:Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025 na kutoa hotuba katika Shirika la Urafiki wa Watu wa China na Nchi za Nje, ambapo pia alitazama video kuhusu "Uhusiano na Kuliang: Tamasha la Kwaya la Vijana wa China na Marekani Mwaka 2025."

Elyn MacInnis, mwanzilishi wa Marafiki wa Kuliang, na Luca Berrone, rafiki wa Rais Xi kutoka Iowa, Marekani walisimulia simulizi zao za Kuliang, mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Marekani na ushirikiano kati ya serikali za mitaa.

Wameelezea upendo wao mkubwa kwa China na shukrani zao kwa Rais Xi kwa kujali kwake vijana wa nchi zote mbili na wamesema pia kwamba wataendelea kuchangia kuhimiza urafiki kati ya Marekani na China.

Wajumbe wa vijana wa Marekani wameelezea hali yao ya kutembelea China, na wamesema wanapenda kuwa mabalozi wa urafiki wa kizazi kipya, na kuenzi simulizi kubwa za urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Katika hotuba yake, Peng amesema kwamba simulizi ya muda wa miaka 100 ya Kuliang na urafiki wa kina wa Rais Xi na marafiki zake wa zamani katika Iowa ulioanzia miaka zaidi ya miaka 40 iliyopita ni kielelezo cha urafiki kati ya China na Marekani.

"Ingawa nchi hizi mbili zina tofauti katika historia, tamaduni na lugha, watu wa China na Marekani wanapenda familia zao na ni wema, wenye urafiki, wachapakazi na wanaofuata hali halisi, ikimaanisha kuwa wanaweza kuwa marafiki na washirika wazuri," amesema.

Peng amesema, katika mwaka mmoja uliopita tangu Rais Xi atoe pendekezo la China la kukaribisha vijana 50,000 wa Marekani kutembelea China, kufanya mawasiliano na kusoma masomo ndani ya miaka mitano, vijana wengi kutoka Marekani wamealikwa kutembelea China na kwamba licha ya kujionea hali halisi ya China, wamepata marafiki wapya na kuandika ukurasa mpya wa urafiki kati ya China na Marekani.

Kabla ya shughuli hiyo, Peng alikutana na MacInnis na Berrone, akielezea shukrani zake kwa mchango wao wa muda mrefu kwa ajili ya mambo ya urafiki kati ya China na Marekani na amewahimiza kuendelea kufanya juhudi za dhati ili kuongeza mawasiliano na maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, akishiriki kwenye shughuli ya Uhusiano na Kuliang: Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025 na kutoa hotuba katika  Shirika la Urafiki wa Watu wa China na Nchi za Nje  tarehe 17 Julai 2025. (Xinhua/Gao Jie)

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, akishiriki kwenye shughuli ya Uhusiano na Kuliang: Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025 na kutoa hotuba katika Shirika la Urafiki wa Watu wa China na Nchi za Nje tarehe 17 Julai 2025. (Xinhua/Gao Jie)

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, akikutana na Elyn MacInnis, mwanzilishi wa ‘Marafiki wa Kuliang’, na Luca Berrone, rafiki wa Rais Xi kutoka Iowa, kabla ya  shughuli ya Uhusiano na Kuliang:Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025, tarehe 17 Julai 2025. (Xinhua/Ding Lin)

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, akishiriki kwenye shughuli ya Uhusiano na Kuliang:Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025 na kutoa hotuba katika ya  Shirika la Urafiki wa Watu wa China na Nchi za Nje, tarehe 17 Julai 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, akiwa  kwenye picha  pamoja na watu walioshiriki kwenye shughuli ya  Uhusiano na Kuliang:Urafiki kati ya vijana wa China na Marekani 2025, tarehe 17 Julai 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha