Israel yashambulia eneo la Ikulu ya rais wa Syria, makao makuu ya jeshi mjini Damascus

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2025

Gari lililoharibiwa baada ya Israel kushambulia Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria na eneo la Wizara ya Ulinzi katika Uwanja wa Umayyad katikati mwa Damascus, Syria, Julai 16, 2025. (Str/Xinhua)

Gari lililoharibiwa baada ya Israel kushambulia Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria na eneo la Wizara ya Ulinzi katika Uwanja wa Umayyad katikati mwa Damascus, Syria, Julai 16, 2025. (Str/Xinhua)

DAMASCUS/JERUSALEM - Ndege za kivita za Israel zilizidisha operesheni zao za mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali kusini mwa Syria jana Jumatano, zikipiga makao makuu ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria na eneo la Ikulu ya rais katikati mwa Damascus.

Mamlaka za afya za Syria zimesema raia mmoja ameuawa, na wengine 18 kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika mji mkuu, ambayo yamejumuisha angalau mashambulizi matano tofauti ya anga yakilenga katikati mwa Damascus.

Picha za video zilizorushwa kwenye runinga ya Syria zinaonyesha moshi ukifuka kutoka Uwanja wa Umayyad, ambako jengo la kamandi kuu ya jeshi linapatikana.

Moshi ukionekana karibu na makao makuu ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria mjini Damascus, Syria, Julai 16, 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Moshi ukionekana karibu na makao makuu ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria mjini Damascus, Syria, Julai 16, 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria limesema sehemu za makao makuu na wizara ya ulinzi zimebomolewa, na mashambulizi mengine yamepiga majengo katika makazi ya al-Malki ya juu na karibu na Kasri la Tishreen. Limesema, hatma ya maafisa waandamizi waliokuwa ndani ya kituo hicho bado haijajulikana.

Msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha operesheni hiyo, akisema kuwa "makao makuu ya jeshi mjini Damascus ni mahali ambapo makamanda wa utawala wa Syria huelekeza operesheni za kivita na kutuma vikosi vya utawala huo kwenye eneo la Sweida."

Katika taarifa hiyo, msemaji huyo ameongeza kuwa "Eneo lengwa la kijeshi karibu na ikulu ya rais wa Syria mjini Damascus limepigwa."

Lori la zimamoto likionekana karibu na jengo lililobomolewa katika shambulizi la anga la Israel kwenye makao makuu ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria mjini Damascus, Syria, Julai 16, 2025. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Kusini mwa Syria, mashambulizi ya Israel pia yalilenga misafara ya vikosi vya serikali na kambi zao katika Jimbo la Sweida, yakiua maafisa waandamizi watatu katika kijiji cha al-Majimer, kwa mujibu wa shirika la uchunguzi.

Aidha, mashambulizi mengine ya Israel yameua watu wengine takriban saba, na kufanya idadi ya waliouawa miongoni mwa vikosi vya serikali kufikia 10. Mashambulizi zaidi yamekumba karibu na mji wa Daraa, kikosi cha 189 mjini Jabab na kikosi cha 132 magharibi mwa Daraa.

Katika maeneo ya nje kidogo ya Damascus, ndege za kivita za Israel pia zimeshambulia mji wa al-Kiswah, ingawa hakuna hasara iliyoripotiwa kwa sasa.

Picha iliyopigwa Julai 16, 2025 ikionyesha jengo la makao makuu ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria lililobomolewa katika shambulizi la anga la Israel mjini Damascus, Syria. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha