

Lugha Nyingine
Wang Yi asema SCO inaweza kuchukua jukumu kubwa zaidi katika utulivu na maendeleo ya kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) Nurlan Yermekbayev mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Julai 16, 2025. (Xinhua/Zhao Zishuo)
TIANJIN - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana Jumatano alipokutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) Nurlan Yermekbayev katika mji wa Tianjin amesema kuwa SCO inaweza kuchukua jukumu muhimu zaidi katika kulinda amani na utulivu wa kikanda wakati huohuo ikihimiza maendeleo na ustawi.
Katika kuelezea shukrani zake kwa juhudi za Katibu Mkuu huyo tangu kushika wadhifa huo, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema kuwa Yermekbayev ametoa mchango mkubwa sana katika kusukuma mbele utekelezaji wa maafikiano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi wanachama wa SCO na ameanzisha uhusiano mzuri wa kikazi na idara mbalimbali nchini China.
Amesema kuwa ikiwa jumuiya jumuishi ya kikanda yenye idadi kubwa ya watu, eneo pana zaidi la kijiografia, na uwezo mkubwa zaidi duniani, SCO inapata ufuatiliaji mkubwa unaoongezeka kutoka jumuiya ya kimataifa, na inaweza kuchukua nafasi muhimu zaidi katika kulinda amani na utulivu wa kikanda huku ikihimiza maendeleo na ustawi.
"SCO inaweza pia kutoa mchango katika kuunda aina mpya ya uhusiano wa kimataifa na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu," Wang ameongeza.
Akisema kuwa Sekretarieti hiyo ndiyo chombo muhimu zaidi cha kudumu cha SCO, Wang ameongeza kuwa chini ya uongozi wa Katibu Mkuu, Sekretarieti hiyo itachukua jukumu kubwa zaidi katika kuhakikisha utendaji wenye ufanisi wa SCO, kuratibu hatua za pande zote, na kuongeza ushawishi wa jumuiya.
"Kama mwenyekiti wa zamu wa SCO, China imeandaa shughuli zaidi ya 90 na kuhimiza ushirikiano mbalimbali," amesema Wang, akitoa wito kwa Katibu Mkuu huyo kuendelea kuiunga mkono China katika juhudi zake za kuandaa mkutano wa kilele ulio wa kirafiki, wa mshikamano na wenye matunda.
Kwa upande wake Yermekbayev amesema, China imependekeza na kutekeleza shughuli muhimu, zikiinua ushirikiano kati ya pande mbalimbali hadi kufikia ngazi mpya.
"Sekretarieti itaendeleza uungaji mkono wake kikamilifu kwa nchi mwenyekiti wa zamu China, kwa pamoja kuwezesha maandalizi ya mkutano wa kilele wa SCO wa Tianjin ili kuhakikisha matokeo yenye matunda," Katibu Mkuu huyo amesema.
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma