GDP ya China yaongezeka kwa asilimia 5.3 katika robo ya 1 huku kukiwa na changamoto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2025

Wateja wakinunua bidhaa kwenye duka la Pangdonglai mjini Xuchang, Mkoani Henan, katikati mwa China, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Jianan)

Wateja wakinunua bidhaa kwenye duka la Pangdonglai mjini Xuchang, Mkoani Henan, katikati mwa China, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Jianan)

BEIJING - Pato la Taifa la China (GDP) limeongezeka kwa asilimia 5.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025 kuliko mwaka jana, takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zimeonyesha jana Jumanne ambapo katika robo ya pili, GDP iliongezeka kwa asilimia 5.2 kuliko mwaka jana.

"Uchumi umepata maendeleo thabiti licha ya shinikizo, huku viashiria muhimu vya uchumi vikifanya vyema kuliko ilivyotarajiwa," amesema Sheng Laiyun, Naibu Mkuu wa NBS, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Jumanne mjini Beijing.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, pato la viwanda la China liliongezeka kwa asilimia 6.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, huku sekta ya viwanda vya vifaa na vya teknolojia ya hali ya juu ikirekodi ukuaji wa haraka.

Aidha, zinaonesha kuwa, soko la watumiaji lilidumisha mwelekeo wa kupanda katika kipindi hicho, huku mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi yakipanuka kwa asilimia 5 katika nusu ya kwanza kuliko mwaka jana. Kasi hiyo imeelezwa kuwa ni asilimia 0.4 kuliko ongezeko lililorekodiwa katika robo ya kwanza.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, uwekezaji wa mali zisizohamishika uliendelea kukua katika kipindi hicho cha miezi sita ya kwanza, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.8 kuliko mwaka jana. Hasa, uwekezaji katika sekta ya viwanda umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Soko la ajira liliendelea kuwa tulivu kwa ujumla, takwimu zinaonesha, huku kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilichofanyiwa utafiti kikiwa wastani wa asilimia 5.2 katika nusu ya kwanza, ikiwa imepungua kwa asilimia 0.1 kuliko robo ya kwanza.

Mapato ya matumizi kwa kila mtu nchini China yalifikia yuan 21,840 katika kipindi cha Januari-Juni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.3 kuliko mwaka jana katika mahesabu ya kawaida, au asilimia 5.4 baada ya kupunguza vipengele vya bei, kwa mujibu wa NBS.

Licha ya kuongezeka kwa changamoto na hali ya kutokuwa na uhakika kutoka nje, China imepata ukuaji thabiti wa uchumi katika nusu ya kwanza ya mwaka (H1) na inachukua hatua kikamilifu kudumisha utulivu na kuendeleza kasi ya ukuaji katika miezi ijayo.

Wateja wakinunua bidhaa kwenye duka la Pangdonglai mjini Xuchang, Mkoani Henan, katikati mwa China, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Jianan)

Wateja wakinunua bidhaa kwenye duka la Pangdonglai mjini Xuchang, Mkoani Henan, katikati mwa China, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Jianan)

Watu wakipiga picha za roboti yenye umbo la binadamu ya Unitree's G1 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Uvumbuzi cha Zhongguancun mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Chen Zhonghao)

Watu wakipiga picha za roboti yenye umbo la binadamu ya Unitree's G1 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Uvumbuzi cha Zhongguancun mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Chen Zhonghao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha