DRC yaeleza nia ya kuhimiza uhusiano wa pande mbili na China kuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa Kusini-Kusini

(CRI Online) Julai 16, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kongo Anatole Collinet Makosso amesema nchi yake ina nia ya kushirikiana na China kuhimiza uhusiano wa pande mbili kupata maendeleo makubwa zaidi, ili kuwa mfano wa kuigwa wa urafiki kati ya Afrika na China, na ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Makosso amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa China nchini humo An Qing jana Jumanne.

Pia amesema nchi yake iko tayari kutimiza jukumu yake ikiwa mwenyekiti wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa upande wa Afrika, na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake An Qing amesema, China inapenda kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili chini ya mfumo wa FOCAC, kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili na mkutano wa kilele za baraza hilo, na kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili kufikia kiwango cha juu zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha