Chama tawala nchini Zambia chasifu ziara yake nchini China

(CRI Online) Julai 16, 2025

Chama tawala nchini Zambia United Party for National Development (UPND) kimeelezea ziara yake ya hivi karibuni nchini China kwamba ni uzoefu wa thamani wa kujifunza, si tu kuimarisha uhusiano na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), bali pia kwa kuchangia maendeleo ya taifa ya Zambia.

Mkurugenzi wa Habari wa UPND Mark Simuuwe amesema, majadiliano yaliyofanyika na maofisa wa CPC yalikuwa ni muhimu katika kuongeza nguvu ya uhusiano kati ya vyama hivyo viwili vya kisiasa na katika kutafiti mikakati ya maendeleo inayoweza kuwa na manufaa kwa Zambia.

Amesisitiza kuwa Zambia ina mengi ya kujifunza kutoka njia ya maendeleo ya China, hususan mkakati wa China wa kuondokana na umasikini kama mfano ambao Zambia inaweza kuutumia katika kukabiliana na changamoto zake za umasikini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha