FOCAC inaendeleza ushirikiano kati ya Afrika na China katika ujenzi wa miundombinu

(CRI Online) Julai 16, 2025

Waziri wa Kazi na Uchukuzi wa Uganda, Katumba Wamala amesema, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) linalotimiza miaka 25 mwaka huu, limeibuka na kuwa jukwaa muhimu kwa nchi za Afrika kutoa sauti ya vipaumbele vyao vya maendeleo na mikakati inayoendana na China kwa ukuaji wa pamoja.

Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua yaliyofanyika Wilaya ya Kayunga, katikati ya Uganda, Waziri huyo amesema FOCAC imeziwezesha nchi nyingi za Afrika kuendeleza miradi ya nishati muhimu na miundombinu ya uchukuzi kwa kuungwa mkono na China.

Amesema Uganda imefaidika sana na ushirikiano unaotokana na FOCAC, akitolea mfano upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, na ujenzi wa Barabara Kuu ya Kampala – Entebbe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha